11/08/2026
Tunapenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika mwisho wa mkutano huu wa injili hapa katika viwanja vya Baranga center Kwa siku zote nane (08). Tumeshuhudia wema wa Mungu katikati yetu, tumemtangaza Yesu Kristo na watu wameokolewa.
Tunamshukuru Mungu pia kwa kila mmoja aliyeshiriki nasi katika mkutano huu aidha waliohudhuria, walioomba, waliohudumu na kwa wote waliotoa mchango wao kwa ajili ya kaz hiii ya Injili. Mungu wa mbinguni awabariki sana.
Utukufu, heshima na sifa zote ni kwa Mungu wetu aliyetuwezesha.
Tutaendelea kuwashirikisha baadhi ya picha za kumbukumbu au matukio yaliyojili katika siku zote za Mkutano wa Injili. Amina!