23/03/2026
SHALOM
Tujifunze pamoja 😇
Isaya 66:9a SUV
[9] Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema Bwana
Isaiah 66:9a NKJV
[9] Shall I bring to the time of birth, and not cause delivery?” says the Lord.
Mungu anakuhakikishia ya kwamba kile alichokianzisha , atakikamilisha..
YES, MUNGU ANAKAMILISHA KILE ALICHOKIANZISHA.
Huu ni moyo wa Mungu kwa watu wake , wakati unapitia kipindi cha kusubiri, maumivu, na matarajio makubwa, rejea katika mstari huo na kumbuka mambo haya
1. Mungu ndiye muanzilishi.
Mungu anaposema, “Nitaleta wakati wa kuzaa…”, anatukumbusha kuwa Yeye ndiye anayeanza mambo katika maisha yetu.
Ndoto ulizo nazo, Wito uliopo moyoni mwako, Maombi unayoendelea kuomba.
These are not accidents. If they are from God, then He Himself allowed them to begin.
2. Maumivu Sio Mwisho
Kuzaa kuna uchungu, lakini uchungu huo hauleti kifo unaleta uzima.
Vivyo hivyo katika maisha:
Changamoto zako unazopitia, kuchelewa kwa majibu, Mapambano unayopitia, si ishara ya kushindwa, bali ni dalili kuwa kuna jambo linaenda kuzaliwa.
3. Mungu Haachi Kazi Yake Katikati
Mungu anauliza swali:
“Je, nitaleta mpaka wakati wa kuzaa nisilete mtoto?”
Jibu ni hapana.
Mungu haanzi kitu kisha aache njiani.
Yeye si k**a binadamu
Hawezi kushindwa kutimiza ahadi zake
K**a amekufikisha hapo ulipo, atakukamilisha
4. Amini Wakati wa Mungu.
Kila kuzaliwa kuna wakati wake sahihi.
Wakati mwingine tunajiuliza:
“Kwa nini imechelewa?”( Wenda umeomba kazi, mtoto, mume,mke, biashara, uponyaji.et
“Kwa nini bado haijatokea?”
Lakini Mungu anafanya kazi kimya kimya.(EVEN IN SILENCE, HE IS STILL WORKING) Anakuandaa wewe na kile ulichobeba.
Kuchelewa si kukataliwa ni maandalizi ya Mungu.
5. Usikate Tamaa Kabla ya Kuzaa( usikate tamaa kabla hujapata kile ulichoomba)
vumilia. yes,
Usiache kuomba
Usiache kuamini
Usiache kusimama katika ahadi ya Mungu
Haujaumbwa kubeba ahadi milele umeumbwa kuizaa ahadi na kuimiliki.(You are not meant to carry a promise forever—you are meant to give birth to it and inherit.😇)
🔥🔥