18/06/2023
JE UMEPOTEZA NAFASI YAKO KWENYE NDOA, MAHUSIANO, KAZI, NA UCHUMI? FANYA HIVI
✍By Mtumishi Fahim 💚Whatsapp 0716 822126💥
NAFASI NI NINI🤔?
Nafasi: ni mahali au eneo ambalo Mungu humpa au kumweka mtu, ili aweze kumfanikisha kwa mafanikio ya kiroho na kimwili,
Pia ni mahali ambapo Mungu akitaka kukutana na mtu anakuja hapo, ili kumbariki na kumwongeza, MWANZO 2: 15-16.
Nafasi yako ndiyo imebeba, (HESHIMA, MUME,/MKE, NDOA, AFYA, KAZI, UCHUMI, AMANI, NA MAFANIKIO.)
Kila nafasi Mungu anayo kupa, ina miiko yake. MWANZO 2: 17. Jitahidi ujue miiko ya nafasi yako na uilinde maana ndiyo imeshikilia hatima yako, k**a hujui miiko ya nafasi yako mwombe Mungu akujulishe na akuwezeshe kuilinda 🙏
Kazi ya shetani nikuhakikisha tunavunja miiko ya nafasi zetu ambazo Mungu ametupa k**a zawadi ya kuishi maisha bora yasiyo na mateso hapa duniani🌏
Mtu anapokuwa nje ya nafasi ni wazi kuwa anapishana na mambo mengi sana ambayo Mungu anakuwa ameyakusudia katika wakati husika. Hakuna kilicho bora kutoka kwa Mungu kinachoweza kuendelea katika maisha ya mwanadamu akiwa nje ya nafasi.
Kila nafasi ina marupurupu yake. Kinachoamua kuendelea kupokea au kusitishiwa marupurupu ni nafasi. Kiongozi yeyote anapoondolewa kwenye nafasi au anapopoteza nafasi aliyokuwa nayo moja kwa moja viambata vya ile nafasi huondolewa kwake.
Haviondolewi kwa sababu hapendwi, la hasha! Ila ni kwa sababu hana vigezo tena. Kupokea hizo posho, nafasi ndio kigezo kikuu cha kufanikishwa na Mungu.
Ukiona mambo hayaendi kabla ya yote jiulize je uko kwenye nafasi ambayo Mungu anataka ukae au kuna mwiko umeuvunja, na umekutoa inje ya nafasi Mungu aliyo kuwa amekuweka?
Mungu anaweza kuwa anakupenda vizuri tu lakini ili akutane na wewe na kuthibitisha upendo wake kwako ni lazima akukute kwenye nafasi yako kwanza.
Inawezekanaje udai mshahara wa meneja wakati wewe ni mwalimu? Mshahara huamriwa na nafasi Uliyo nayo Kwa hiyo.
Ukiutaka mshahara wa meneja, basi unatafuta kwanza nafasi ya umeneja, mshahara utakufuata wenyewe. Sijui tunaelewana hapo?
Baada ya Adamu na Eva kukosea katika ulimwengu wa roho walipoteza nafasi yao.
✍️ Mwanzo 3:9, “Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?”
Mungu anapouliza Adamu UKO WAPI haimaanishi alikuwa hajui walipojificha. Isipokuwa hakumuona Adamu kwenye nafasi aliyokuwa amemuweka. Ni nafasi ambayo Mungu alikuwa anakutana nao kila alipowatembelea.
Mungu alipowatembelea hakwenda mahali walipojificha bali mahali alipokuwa amewaweka.
Hawakuwa nje ya Edeni, ila nje ya nafasi waliyowekwa na Mungu wakiwa ndani ya Edeni.
Kwa hiyo unaweza kuwepo Kanisani na unahudhuria kila ibada lakini upo nje ya nafasi aliyo kuweka Mungu.
Malanyingi maamzi ya mihemko, visasi au kukulupuka ndiyo yanatuweka inje ya nafasi Mungu alizo tuweka.
Inawezekana Mungu amekupa nafasi ya Mume au mke sahihi, akakosea k**a mwanadamu ukaamua maamzi ya kumlipiza usalirit au kumwacha, tayari umetoka kwenye nafasi yako na huwezi kupokea tena baraka ambazo Mungu alikuwa akiwabariki kwenye ndoa au hayo mahusiano.
Watu wengi, wako kwenye (ndoa kazi biashara mahusiano) na nk. Lakini hawako kwenye nafasi ambazo Mungu amewaweka. Wengi tumeamua maamzi kwa fulsa, vigezo, uzuri, kushawishiwa, MWANZO 3: 6.
Na tume kataa vile Mungu alivyo tupa kwa sababu ya makosa au mapungufu fulani tukajikuta tumejiingiza kwenye maumivu zaidi na kupoteza nafasi zetu mbele za Mungu. MWANZO 3: 7.
Kuna tofauti ya kuitwa jina la nafasi na kukaa kwenye nafasi. Kuitwa jina la nafasi haina tofauti na kuitwa jina la cheo. Sio kila mwenye cheo basi anakitendea haki cheo husika. Umewahi kusikia watu wanasema pengo lake halitazibika? Au bado hajapatikana mtu anayeweza kuvaa viatu vyake? Wanachojaribu kuzungumza ni suala la kukaa kwenye nafasi ipasavyo...
HABARI NJEMA💥
Kila nafasi uliyo ipoteza inaweza kurejeshewa kwa toba na kumwomba Mungu kupitia Yesu Kristo, ambae yeye ni njia na upatanisho kati ya mwanadamu na Mungu 🙏
MAOMBI YA UREJESHO WA NAFSI
Mungu baba, naomba uni rehem na kunisamehe makosa yangu niliyo kukosea kwa kujua na kutokujua, nilikaidi njia zako, nikapoteza nafasi yangu uliyo nipa ili kuishi maisha ya sahihi uliyo nipangia wewe, naomba unisamehe na kunirejesha kwenye nafasi yangu kupitia mwanao Yesu Kristo 🙏
Naomba; urejesho wa ndoa yangu iliyo potea, kwa jina la Yesu 🙏
Naomba; urejesho wa afya yangu iliyo potea, kwa jina la Yesu 🙏
Naomba; unirejeshee upendo ulio potea kwa Mume wangu au Mke wangu, kwa jina la Yesu Kristo 🙏
Naomba; urejesho wa pesa na uchumi wangu ulio potea na kuibiwa na shetani kwa sababu ya mimi kutoka inje ya nafasi na kusudi lako, kwa jina la Yesu 🙏
Naomba; unirejeshee nyota na kibali cha maisha yangu nilichopoteza kwenye mambo mbali mbali, kwa jina la Yesu 🙏
Naomba; urejesho wa ibada yako ndani yangu nipate kibali cha kukuabudu na kukubalika mbele zako, unitakase kwa damu ya Yesu iondoe kila kinachoweza kuzuia mahusiano yangu mimi na wewe Mungu kwa jina la Yesu 🙏
NIMEOMBA YOTE KUPITIA MWAONAO YESU KRISTO, AMINA🙏
Mungu akubariki 🙌
Kwa maombi na ushauri nitumie ujumbe 💚Whatsapp 0716 822126 .
✍by Mtumishi Fahim 0716 822126 💥