Paza sauti

Paza sauti Lengo kueneza Neno la Mungu, mafundisho ya kweli, na mahusiano ya kuwajenga watu kiroho na kimwili. na kuishi maisha yanayompendeza Mungu.

15/03/2026
05/02/2026

NINAWEZA KUOA /KUOELEWA NA MTU ASIYEOKOKA

NINAWEZA KUOA AU KUOLEWA NA MTU ASIYEAMINI (ASIYEOKOKA)..?
Leo ningependa kungalia upande wa kuoa /kuolewa na mtu asiyeamini, k**a kijana unaweza ukawa umekutana na swali hili ambalo tutaenda kuliangalia kwa upana wake na k**a si wewe basi hata ndugu au rafik yako wa karibu anaweza akawa yupo kwenye kipindi cha kujiuliza swali hili.
Katika mazingira au jamii yetu tunakutana na watu wa aina mbalimbali kipindi tukiwa mashuleni, vyuoni, kazin au sehemu nyingine katika jamii, na katika mazingira hayo tunaweza tukajikuta tukiwa tumependa watu ambao si wa imani yetu, s watu waliokoka. Je tunafanyaje? Na tukiangalia tunapendana sana na hakuna shida yoyote kati yetu isipokuwa utofaut wa imani zetu tulizonazo.
Biblia inasemaje kuhusu hili?
Naomba nianze kwa kunukuu andiko hili 2 WAKORINTHO 6:14 - 18,tutaangalia mstar 14 & 15,
"Msifungiwe NIRA pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa kwa maana pana urafik gani kati ya HAKI na UASI? ,
'Tena pana shirika gani kati ya NURU na GIZA? Tena pana ulinganifu gani kati ya KRISTO na BELIARI (ufisadi)?
' AU YEYE AAMINIYE ANA SEHEMU GANI PAMOJA NA YEYE ASIYEAMINI? "
Maandiko hayo yanazungumzia habar ya mtu aliyeokoka kuoa au kuolewa na mtu asiyeokoka, Neno NIRA limetumika kuelezea muunganiko wa mwanamke na mwanaume wa ndoa.
Nira ni kitu ambacho kilitumika kuwaunganisha wanyama (hasa ng'ombe) kwa kuwafunga kitu hicho shingoni ili waweze kwenda kwa pamoja bila kuachana mara nying hutumika katika kilimo ili kuwafanya wafanye Kazi hiyo pamoja, hata k**a mmoja akichoka basi Nira hiyo itamfanya aendelee na Kazi kwa kulazimishwa na mwingine, Hivyo Nira unaweza pia ukaiita ni KIFUNGO kwa kuwa kinamkosesha uhuru wa mmoja kati ya wanyama hao kufanya maamuz yake binafsi.
Kupitia Nira wanyama wawili wanakuwa si wawili tena bali ni mwili mmoja. Ukiangalia kwa ukaribu Nira inavyotumika ni sawa na neno NDOA tunavyolitumia pindi watu wanapounganishwa madhabahuni.
Baada ya ndoa watu wawili wanakuwa si wawili tena bali ni mwili mmoja, baada ya ndoa mmoja hata k**a akitokea amechoka kuendelea na ndoa hiyo si rahisi kutoka kw sababu ndoa imewaunganisha na hairuhus kuachana, Hivyo hapa pia NDOA unaweza ukaiita KIFUNGO k**a tulivyoona NIRA ilivyotumika, na ndio maana ndoa huitwa kwa jina lingine PINGU ZA MAISHA.
Kutokaa na andiko tulilolisoma hapo juu ni wazi kabisa hatutakiwi kufanga ndoa au kufungiwa Nira na mtu ASIYEAMINI /ASIYEOKOKA. Najua unaweza ukawa upo kwenye uhusiano na mtu ambaye HAJAOKOKA na unampenda sana hivyo kwa kusema hivi ninaweza nikawa nakuumiza sana moyo wako na kukukatish tamaa, lakini sina jinsi k**a huu ni UKWELI sina budi kuuleza k**a ulivyo bila kificho ili nikusaidie usimkosee Mungu, na kwa kufanya hivyo nitakuwa nimekusaidia pia Mungu atanibariki kwa kuiokoa Nafsi yako iliyo ya THAMANI SANA mbele zake.
Tangu katika agano la kale Mungu akiwakataza watu wake wasioe au kuolewa na watu wa jamii nyingine nje ya Israel, k**a ilivyo sasa tusivyotakiwa kufanya hivyo
Hata Ibrahimu alipotaka kumtafutia mke mwanae Isaka alimuagiza mtumishi wake kwa kumuapiza kuwa asiende kumchukulia mke katika jamii ya watu ambao si wa nyumban kwake,
MWANZO 24 :1-4
"Basi Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi na BWANA alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote. Ibrahimu akamwambia mtumishi wake mzee wa nyumba yake aliyetawala vitu vyake vyote,
'TAFADHALI UUTIE MKONO WAKO CHINI YA PAJA LANGU NAMI NITAKUAPISHA KWA BWANA, MUNGU WA MBINGU NA MUNGU WA NCHI KWAMBA HUTAMTWALIA MWANANGU MKE KATIKA BINTI ZA WAKAANANI AMBAO NAKAA KATI YAO,
'BALI ENENDA HATA NCHI YANGU NA KW JAMAA ZANGU UKAMTWALIE MWANANG ISAKA MKE "
(ni vizur ukisoma sura yote......)
Hivyo swala la kuoa /kuolewa nje ya watu wa jamii yetu (waliokoka) ni KINYUME cha Neno na mapenzi ya Mungu. Unaweza ukawa ulishasikia hili, lakini labda unajiuliza ni kwanin Mungu akataze? Shida ipo wapi? Naomba nikaelezee sababu k**a 4 hivi :
(1). KUZAA MATUNDA.
Mungu alipotuchagua, alkusudia tumzalie matunda katika wokovu wetu na hii ndio sababu ya sisi kuwepo duniani.
YOHANA 15 :16,
"SI ninyi mlionichagua mimi bali ni mimi niliowachagua ninyi nami nikawaweka mwende MKAZAE MATUNDA na matunda yenu yapate kukaa ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. "
Pia ukisoma katika MWANZO 1 :28, alipomuumba Adam na Hawa aliwaambia ZAENI mkaongezeke, hapa alikuwa hamaanishi tu kuzaa watoto na kuongezek kwa idadi ya kawaida bali alikuwa anamaanisha KUZAA NA KUONGOZEKA KIROHO.
Mungu anapokupa mke au mume haangalii tu mwende mkazae watoto wa kimwili bali pia huangalia KUSUDI lake alikoweka ndani yenu la kitumishi, Hivyo huangalia matunda yenu mtakayozaa kiroho pindi mkiwa pamoja.
Si kila mtu anaweza akakusaidia kutimiza kusudi la Mungu ndani yako, Hivyo unabidi utulie ili akupe mtu sahihi. Hata k**a ameokoka si sababu ya yeye kukufanya umtumikie Mungu k**a yeye alivyopanga.
Sasa kwa mtu asiyeokoka ni WAZI kabisa hawezi kukusaidia katika hili.
(2).MWILI WAKO NI HEKALU LA MUNGU
Miili tuliyonayo ni hekalu la Mungu kwa kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yetu hivyo hatuwez tukaangunisha miili yetu ambayo ni hekalu la Mungu na miili ya watu wasiokoka ambayo ni hekalu la miungu mingine. Kufanya hivyo ni dhambi na chukizo mbele za Mungu.
Kumbuka hekalu ni sehemu /nyumba ya ibada hivyo huwezi ukamchanganya Mungu na miungu mingine katika ibada ya pamoja, ni lazima mmoja kati yao aondoke. Usisahau pia watu wakiwa kwenye ndoa wanakuwa mwili mmoja yaani unachanganya mwili wako ambao ni Mtakatifu na mwili wa mtu mwingine asiyeokoka ambao usiomtakatifu.
Soma 1 WAKORINTHO 6 :19
(3).NDOA INA NGUVU YA KUGEUZA MOYO WAKO.
K**a ukioa au kuolewa na mtu ASIYEAMINI kuna uwezekano mkubwa wa wewe kushindwa kumwabudu Mungu na kuacha WOKOVU.
Mfalme Sulemani alipoanza kumtumikia Mungu alikuwa na juhudi na moyo wa kumpenda sana Mungu lakini alipokuja kuoa wanawake wageni (wasiookoka) aliacha kumtumikia Mungu wa kweli na akatumikia miungu migeni ya wake zake.
Soma 1 WAFALME 11 :1-3.
(4).NDOA INA NGUVU YA KUKUFANYA UENDE MBINGUNI AU JEHANAMU.
Ndoa si kitu Cha kuchezea, si kitu Cha majaribio, ndoa itakufanya uende mbinguni au ukose kumuona Mungu. Hivyo usijaribu KURAHISISHA UAMUZI wako wa nani wa kuingia nae kwenye ndoa.
FIKIRI KWA MAKINI, AMUA KWA BUSARA.
*********//*********, ***//, ********
K**a upo kwenye ndoa ukiwa bado wote hamjaokoka lakini baadae ukawa umeokoka maandiko yanasema usimuache mwenzako hata k**a yeye hajaokoka k**a yupo tayar kuendelea kuwa na wewe. 1 WAKORINTHO 7 :12-16.
Na k**a ulifanya kosa la kuoa /kuolewa na mtu asiyeokoka ukiwa wewe upo kwenye wokovu, INABIDI utubu dhambi hiyo kisha utafute msaada zaidi kwa watumishi wa Mungu.
Na kwa wale ambao wameokoka ila wana wachumba ambao hawajaokoka, si mimi bali Mungu anawaambia MSIFANYE KOSADHAMBI YA MAKUSUDI YA KUOA AU KUOLEWA NA MTU ASIYEAMINI
EZRA SURA YA 10 (soma hapa)
Ni kweli unampenda sana na yamkini mmetoka nae mbali lakini kumbuka upendo wako kwa Mungu UNAPASWA kuzid upendo wako wa kibanadamu na Yesu umetoka nae mbali kuliko huyo mpenzi wako.
Amekuahidi atabadilisha dini? Ndugu wokovu si DINI ila ni KUCHAGULIWA, ni UTAKATIFU KATIKA KRISTO YESU.
SHINDA MOYO WAKO, FANYA UAMUZI SAHIHI.
SIKU ZOTE MOYO NI MDANGANYIFU...!
USIUCHEZEE WOKOVU WAKO.

04/08/2025

In history that I have gone through with this friend of mine, I find myself falling for him so much🥰…..GOD TAKE CARE OF YOU SO MUCH.

28/05/2025

MWAMBIE MUNGU ASANTE

Mwambie Mumgu asante Kwa wema wake kwako hata k**a hujui ni kitu gani amekutendea we mwambie asante kwani kuna mengi ametenda bahati mbaya macho yako hayaoni.

Biblia ina tushari kumwambia Mungu asante Kwa kila hali tunayo ipitia maishani mwetu hata k**a ni hatua chungu kwetu lakini inatupasa kujua kuwa Mungu amefanya hayo Kwa sababu anatupenda na ni Kwa afya na faida yetu wenyewe, tunasoma 1 Wathesalonike 5:18
[18]shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

Aisee mwambie Mungu asante!.

Mungu anasema 1 Petro 5:7 [7]huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Ndiyo Mungu hujishughulisha Sana nambo yako, Ile kwamba hauoni haimanishi hajisghulishi na mambo yako jua bado anahangaika Sana kuhakikisha unapata mahitaji yako.

Angalia Leo hii Una mwaka hujafika hospital kabisa nawe ni shahidi ukienda hospital Una kuta watu wamelala hawajiwezi unadhani wewe ni mjanja kukwepa bacteria wa magonjwa hata uwe mzima Leo hii?.

Aisee mwambie Mungu asante.

Tazama Vizuri ona wapendwa wametwaliwa pikipiki zimewapitia lakini wewe kila siku wapanda pigipiki je ni kweli mpaka hapo huoni cha kusema asante Kwa Mungu wako. haikubaliki kabisa hebu kuwa Makini kidogo mwambie Mungu asante.

unajua wakati fulani unaweza kudharau kitu lakini usijue Mungu amehangaika mmno mpaka wewe ukapata japo hukidhamini. Biblia inatupa mfano mmoja mzuri Sana unao patikana katika 1 Wafalme 17:5-6
[5]Basi akaenda akafanya k**a alivyosema BWANA; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani.
[6]Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.

Hii nu habari ya Eliya hebu tutafakari pamoja tuone jinsi Mungu anavyojishughulisha na maisha yetu. Ona kulikuwa na njaa Kali Sana kiasi kwamba Mito ilikuwa imekauka sasa jiulize hivi kungulu aliutoa wapi ule mkate na Ile nyama kila siku. Halafu Kwa nini kungulu mwenyewe hakula ikiwa kulikuwa na njaa nchi zima, je Nani huyu alikuwa na shibe nyingi kiasi cha kutupa mkate na nyama kila siku?. Nini naona hapa ni kuwa kile chakula hakikuwa cha kimwili hapana Bali kiliandaliwa na Mungu mwenyewe si unakumbuka aliwahi kuwapikia waisraeli Mana jangwani. Tena kumbuka kuwa Elia aliwahi kuletewa mkate na gudulia la maji na malaika ( 1 Wafalme 19- 8 ) Kwa hiyo usishangae nikikuambia Mungu alimwandalia Elia chakula na kukijifikisha kwake Kwa njia ya kungulu.

Hallelujah!. Eliya angeweza kudharau kile chakula ukizingatia kimeletwa na kungulu,sote tuna mfahamu vizuri kungulu kuwa si msafi, Eliya angewza kusema Mimi ni mtumishi mkubwa wa Mungu siwezi kulishwa na kungulu lakini tunaona Eliya alipokea Kwa shukrani.

Mpendwa inawezekana kweli umelalia vipande vya mhongo nawe Una maswali kwanini ule mihongo wewe ni mtumishi, sikia ndugu yangu mwambie Mungu asante hata Kwa hiyo mihogo maana Mungu amehangaika Sana kuhakikisha wewe unaipata hiyo mihogo nakwambia mwambie Mungu asante. kuna watu hata mhogo wamekosa siku ya Leo.

jifunze kumwambia Mungu asante atakubarikia mihogo yako utashangaa, pengine hunielewi angalia mezani kwako Leo Una ungali na matembele tuu lakini Kwa jirani yako mezani kuna mbonga Saba na matunda kibao na ni kila siku lakini ajabu ni kwamba wewe Una afya Bora kuliko yao, unaelewa lakini ?,mwambie Mungu asante. Rafiki jirani yako ana gari zuri lakini angalia jinsi wanavyo gombana kila siku lakini wewe na mwenza wako mnajipia kiwali chenu tena hata mafuta hamna mwaongazana kanisani , mara sokoni mna Amani Tele mioyoni mwemu,mkifika mahali mnanunua mahindi ya kuchoma ndiyo soda yenu mnakula huku mkitembea na malove kibao kila anye watazama anatamani aipate ndoa yenye furaha na amani k**a yenu. Huoni kuwa ni ajabu.

Asisee mwambie Mungu asante.

kuna wakati mwingine Mungu anawainua watu hata Wale ulifikiri hawawezi kukusaidia Kwa sababu hawana uwezo, japo hawana kitu wanajinyima kichache walicho jaliwa kukusaidia.

Hebu angalia kisa cha Elia kutunzwa na Yule mama mjane. Utakubaliana NAMI kuwa si Jambo la heshima mwanaume mzima kutunzwa na mwanake tena mjane haiingii akilini kabisa hasa Kwa utamaduni wetu tena Kwa upande wake Eliya alikuwa nabii ambaye Mungu aliweza kujibu maombi yake Kwa Moto lakini Mungu aliruhusu atunzwe na mwanamke mjane sijui unapo jaribu kukaa mahali pa Eliya unajisikiaje wewe lakini kwangu maswali ya yasingekoma wapi Mungu ninaye yemtumikia yasimgekosekana. Eliya aliyapokea haya yote Kwa shukrani.

Mpendwa kuna mengi sana ambayo Mungu anafanya katika maisha yetu hata hatuelewi Kwa nini amefanya Kwa sababu tunaona either ametuonea au hatukustahili tutendewe vile sababu Sisi ni Wana wa ufalme lakini Biblia inatuambia yeye Mungu amejishughulisha Mno na maisha yetu mpaka tuko hivi.ni Kwa kulijua hili kuwa uwezo wetu wa kutambua ukuu na wema wake Mungu maishani mwetu ni ndogo ndio maana Biblia imetushauri tumahukuru Mungu Kwa kila Jambo maishani mwetu.

Mwambie Mungu asante.

Katika jina la Yesu nasema na wewe sasa ambaye umeachwa na mchumba wako futa machozi mwambie Mungu asante iko nguvu katika kushauru utaona Mungu akigeuza machozi yako kuwa kicheko kumbuka wale 10 wenye ukoma mmoja wao alipo Rudi kushauru akapokea uponyaji kabisa wa mwili wake. Iko nguvu katika kushauru nasema nawe uliye fell mhtihani wako na sasa umebaki kumlaumu Mungu nakuambia Kwa jina la Yesu geuka!. badili mtazamo wako Anza kusema asante Kwani iko njia amekuandalia utafika chuoni tu.Mungu aweza kumfanya yasio wezekana.

Ushuda:
Namfahamu dada mmoja aliye kuwa kafel kidato cha nne , akarudia mtihani mara SITA ili aweze kupata alama za ufaule andelee mbele lakini hakufanikiwa. Dada huyu alikuwa mkarimu mno alifikia pahala pa kuwa saidia rafiki zake wenye mazingira magumu kwa kuwaombea sehemu ya kulala rafiki zake kwa wazazi wake ili wasome pamoja na yeye ndiye mara nyingine aliwaelekeza wezake lakini matokeo yakitoka yeye amefel na wezake wanafaulu.

Ndipo alipoamua kumshukuru Mungu juu ya maisha yake na vile Mungu ameyapangilia, akamwambia Mungu nimefanya kila niwezalo Kwa nguvu zangu ili nami nifanikiwe maishani niliamini njia pekee ni ya kufaulu mtihani huu hakika Mimi nimeshindwa lakini sasa nimekubali kuwa wewe Una njia nyingi za kunifanikisha maishani mwangu Asante Mungu.

Ndipo lilipo mjia wazo la kusoma certificate ya ualimu grade A,nakuambia alifaulu kule ajabu na baada ya hapo akachukua vile vyeti akaenda ili akasome certificate ndipo asome diploma badaye lkn ajabu kule alikataliwa kusoma certificate akapelekwa moja Kwa moja kusoma diploma Leo nakuambia amemaliza degree yake na k**a ni miongoni mwa wasomao ujumbe nina hakika atacomment hapa kudhibitisha maneno haya.

Inuka Baba inuka mama mmekosa mtoto muda mrefu mmesikia maneno ya kila namna Sawa lakini leo neno hili lifanyike unabii kwako badili kilio chako kiwe shukrani Yesu atafanya zaidi ya uwazayo wewe. Hilo lililo mbele yako ni kweli ni kubwa lakini bado Mungu hajashindwa

MWAMBIE MUNGU ASANTE!.

Waweza pia kusambasa ujumbe au kuwafahamisha na wengine juu ya ukrasa ili Kwa pamoja tuweze kutangaza upendo wa Mungu Kwa wengine, usisite kulike ukrasa huu. Waweza kuyapata somo hili na mengine mengi Kwa lugha ya kiengereza kupitia tovuti yetu
https://nenoministry.blogsport.com.

Mhimu.
Usisahau kutuombea Kwa Mungu Baba ili tujaliwe Neema ya kuzijua na kuzinena Siri za Mungu Kwa ujasiri.Nasi tunakushauri Mungu akutimizie haha za moyo wako Sawa na uwingi wa Neema yake katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Na Mwl.
Samuel A. Mwakatajila
Neno ministry@ 2020.

_"Neno la kutia moyo wakati wa matatizo na changamoto hata likiwa la sekunde Moja, lina thamani kubwa  zaidi ya saa moja...
18/05/2025

_"Neno la kutia moyo wakati wa matatizo na changamoto hata likiwa la sekunde Moja, lina thamani kubwa zaidi ya saa moja na zaidi ya maneno ya sifa yatolewayo kwenye raha na mafanikio"*_

Je, unawatia Watu Moyo wakati wa shida Au unawasifu na kuwapongeza wakati wa mafanikio tu?

jifunze kuwatia moyo watu wakati shida hii ni nzuri sana

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255765777744

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Paza sauti posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Paza sauti:

Share