Eben-Ezeri El Elohe Israel For All Nationals

Eben-Ezeri El Elohe Israel For All Nationals Grace of God,Power of healing from heaven, Word of God and deliverance

22/05/2026

KONGAMANO KUBWA LA SIKU NNE ZA KUKUTANA NA DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA NA MARADHI YOTE "' YESU KRISTO '""


KUANZIA SIKU YA TAR; 28/05/2026 HADI TAR; 31/05/2026 WATU WA DINI ZOTE NA MATAIFA YOTE MNAKARIBISHWA .

HIVYO USIKIAPO SAUTI HII NA KUTAMBUA HABARI NJEMA YA UPONYAJI HUU MWAMBIE JIRANI YAKO ALIYE MGONJWA NA WENYE SHIDA MBALIMBALI KUWA WEWE SIYO KIBEGA AU STORE YA MAGONJWA YA SHETANI NA WACHAWI -- HIVYO TWENZETU KWA YESU TUKAONDOLEWE MIZIGO YA MAGONJWA NA MATESO YA SHETANI KUPITIA MTUMISHI WA MUNGU ALIYEPEWA NEEMA NA KARAMA YA UPONYAJI
""PROPHET JACKSON MAAJABU YA MUNGU""

NENO LA MUNGU LINASEMA HIVI KATIKA

Mathayo 14:35-36
[35]Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi;
[36]nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.

UPAKO HUU UTAKUWA NDANI YA HEMA LA UPONYAJI JEHOCIFONA MINISTRIES ILIYOPO MKABALA NA SHULE YA SHILELA SECONDARY GEZAULOLE BOMANG'OMBE HAI KWA MAWASILIANO ZAIDI CALL; 0764304342

Wimbo " Solomon mkubwa "Wewe ni mwema""

02/04/2026

SOMO; UFAHAMU WA ROHONI JUU BARAKA ILIYOPATIKANA MSALABANI KUPITIA DAMU YA YESU KRISTO NA FAIDA ZAKE

""PASAKA hii ni zamu yako ya kutoka utumwani na kwenye vifungo mbali mbali vya siri jifunze pamoja nasi""

A... Nini maana ya pasaka kibibilia!!?
PASAKA ni Jina la aina ya Sadaka na siyo sikukuu ya kula na kunywa K**a wengi wanavyofikiri!
1Korintho; 5:7
KUTOKA 12:1-13

B.... PASAKA ni siku au Mlango wa kutoka kwenye utumwa wa magonjwa-- vifungo--mateso/ magerwza ya kiroho/laana za kichawi nk. maana aliyekushikilia atahukumiwa na Bwana
KUTOKA 12:1-14

C... PASAKA ni Mlango wa ufufuo wa vilivyokufa maishani mwako; ndoa--uchumi-- afya-- kazi za mikono-- familia--ufugaji kilimo nk.


🔍 Maana ya Ufahamu wa Rohoni
Ufahamu wa Rohoni ni uwezo wa roho ya mwanadamu kupewa nuru na kuelewa mambo ya Mungu, ulimwengu wa roho, na ukweli wa ndani ambao hauonekani kwa macho ya kawaida.

Kwa lugha rahisi:
👉 Ni uelewa unaotoka kwa Roho Mtakatifu, sio akili ya kawaida (logic ya kibinadamu)

1--- Ufahamu juu ya damu ya Yesu Kristo iliyotoka kichwani kwa kutobolewa na taji ya miiba na faida zake (baraka za msalaba kutokea kichwani)

MATHAYO 27:/51-53

A... Damu hiyo ya kichwani;ilibeba nguvu au upako wa kuondoa laana na adhabu ya Mungu juu ya ardhi iliyolaaniwa kwa sababu ya dhambi ya kutokukutii sauti ya Mungu pale edeni

MWANZO 3:17

MATHAYO 27:29-31

B... Damu ya Yesu Kristo iliyotoka kichwani pia ilibeba nguvu au upako wa kuondoa adhabu ya kiuchumi/kifedha kwa sababu ya dhambi ya kutokutii Neno la Mungu na kulitekeleza

MWANZO 2:15-17

C... DAMU ya Yesu Kristo iliyomwagika kutoka kichwani ilibeba nguvu au upako wa urejesho wa nguvu ya ufahamu wa kimungu-- nguvu ya kiakili-- maamuzi ya kimungu na mawazo ya kimungu

KOLOSAI 3:1-3

Maana Kuna mambo adui huyafanya kwenye akili ili kubana akili-- ufahamu--maamuzi --mawazo na fikra za mtu wa ndani

2Kor; 4:3-4

2Kor; 11:3

Mwanz; 3:1-15

Kumbuka watu wenye ufahamu--maarifa akili za ubunifu ndiyo watu wanaolipwa mishara mikubwa duniani hivyo ni muhimu Pasaka hii ufufuke kiakili--kiufahamu-- kimaamuzi --kifkra na kimawazo; hizo ndizo faida ya damu ya pasaka iliyobeba baraka za msalaba na faida zake

""MAOMBI YA KIPENGELE HIKI"'

Ninakushukuru Mungu uliye Hai kwa kumtoa mwanao wa pekee; Yesu Kristo aliye Hai--- kwa ajili ya Kuitoa dhabihu na sadaka ya pasaka Kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu; na kila laana na Kila adhabu ya kutokulitii Neno lako juu ya ardhi mama iliyonizaa; ardhi mama ninayoishi na kuifanyia kazi/biashara nk. Ee Bwana nirehemu na kunisamehe mtumishi wako (taja majina yako K**a utambulisho wako wa kiroho) .......... maana damuni mwako nimepokea msamaha wa dhambi na Ukombozi tangu Leo; naialika na kuilekeza damu ya msalaba iliyotoka kichwani mwa Yesu iniondolee adhabu na laana ya kula kwa jasho -- laana ya michongoma na miiba toka Kwa Mungu; laana; Laana ya zuio la kiuchumi na kifedha laana iliyokaa kihalali ya juu ya uso wa ardhi mama iliyonizaa umeniondolea leo kwa sadaka ya pasaka sawa sawa na Neno lako la 1KOR 5:7

MWANZO 3:17 MWANZO 2:15-17 Na damu hii iliyomwagika kutoka kichwani pako inirejeshee nguvu ya ufahamu-- nguvu ya kiakili-- nguvu ya kimaamuzi -- nguvu ya kifikra na kimawazo ; inirejeshee tena utukufu wako ulioniondolea Kwa sababu ya dhambi ya asili ya babu yetu Adam wa kwanza; Yesu pia kwa Kuniondolea zuio la kiuchumi-- kupitia Damu ya msalaba toka kichwani mwa Yesu Kristo tangu Leo sitakula Kwa ajili jasho wala michongoma na miiba haitakuwa sehemu ya kazi ya mikono yangu

"" WAEFESO 1:7

Sali Sala hiyo Kwa Imani Kisha kesho nitakuletea faida ya pili kutokea msalabani kutokana na damu na maji yaliyotoka ubavuni mwa Yesu;

Imeletwa kutoka madhabahu ya JEHOCIFONA MINISTRIES chini ya mpakwa mafuta wa Bwana; Apostle & Prophet Jackson Nelson Nyantamba pia unaweza kuwasiliana Moja Kwa Moja kwa 0764-3043-42 kwa msawali na majibu zaidi

24/12/2025

Madhabahu ya Sauti ya Uponyaji Kilimanjaro Tanzania iliyopo
chini ya Apostle & Prophet Jackson Maajabu Ya Mungu...a.k.a
(Voice of Healing Kilimanjaro) inakukaribisha katika ibada ya mkesha wa kuvuka mwaka kabla ya kuvuka Leo J/tano jioni ya saa tatu usiku usipange kukosa
Njoo na familia yako na ndg; jamaa; rafiki jirani tuabudu pamoja na kupokea Neno la unabii wa mwaka 2026 ili kupokea baraka za kiroho; tupo mkabala na geti la Shule ya Shilela Secondary gezaulole
YOH; 1:3
Call; 0764-30-43-42
Call; 0714-29-54-05

Address

48000
Boma La Ngombe

Telephone

+255764304342

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Eben-Ezeri El Elohe Israel For All Nationals posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Eben-Ezeri El Elohe Israel For All Nationals:

Shortcuts

Share