23/03/2020
-Tarehe 23/03/2020
-Siku: Jumanne.
- Muda: 00:21
-By Pastor & Prophet
Bash*te B. Kado.
"MAOMBI MAALUMU KWA AJILI YA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA, AFRIKA NA DUNIA NZIMA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UGONJWA WA CORONA (COVID-19)"
Utangulizi:
Mungu wetu ni wa rehema, anatambua majira, na nyakati
Imeandikwa katika ile
Zaburi 46:1-4 ikisema
"Mungu kwetu sisi ni kimbilio na Nguvu ni msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso"
-Maana tupo katika kipindi Cha mateso, ni kipindi cha Mungu wetu kuwa kimbilio letu.
Watanzania tuamke tuliombee Taifa letu na nikiwa K**a mtumishi wa BWANA Ninaomba tushirikishane katika maandiko yafuatayo.
Covid-19 (Corona virus.)
HALITALISHINDA KANISA:
Mathayo 16:16-19.
"...Simon petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai,
-Yesu akajibu Akamwambia Heri wewe simoni Baryona kwa kuwa Mwili na damu havikufunuliwa hili bali Baba yangu aliye mbinguni.
-Nami nakuambia 'wewe ndiwe petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu Wala milango ya kuzimu HALITALISHINDA."
-Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni na lolote utakalolifunga Duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lolote litakalofunguliwa Duniani litakuwa limefunguliwa na mbinguni"
MAANA YAKE NI NINI!?
-Ugonjwa wa Covid-19 (corona virus) ni mlango wa kuzimu hivyo Kanisa lazima liushinde katika Jina la Yesu,
-Kanisa limejengwa juu ya mwamba na hakuna Covid-19 (Corona virus) litaiweza kanisa Hilo haliwezekani hata kwa dawa.
-Ninasimama K**a Mtumishi wa BWANA kuwa Covid-19 (Corona virus) haiwezi kulifunga kanisa Bali kanisa litaifunga Covid-19 (Corona virus) katika Jina la Yesu.
-Pia tunakwenda kusimamia katika kile kitabu Cha
2Wakorintho 10:3-5.
"Maana ingawa tunaenenda katika Mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili,
(Maana silaha za vita vyetu si za mwili Bali Zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome).
-Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.
Covid-19 (Corona virus) ni ngome ya adui kudhoofisha utendaji wa BWANA katika Ibada na makanisa ya Mungu.
-Hivyo tunaangusha ngome zote za Virusi hivi vya Corona katika Jina la Yesu.
-Kila fikira iliyojengwa kupitia hili Gonjwa la Covid-19 (Corona virus) tunaiteka katika Jina la Yesu.
-Na kuanzia sasa hii Covid-19
(Corona virus) ninaiamuru kutii Jina la Yesu.
2Nyakati 20:5-9.
"Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalem, nyumbani mwa BWANA, mbele ya ua mpya, Akasema Ee BWANA Mungu wa Baba zetu si wewe uliye Mungu mbinguni?!
-Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa?!
-Na mkononi mwako mna uweza na Nguvu asiweze mtu yeyote kusimama kinyume chako.
-Si wewe Ee Mungu wetu uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele?!
-NAO Walikaa humo, wamekujengea patakatifu pa Jina lako humo wakisema,
'Yakitujia mabaya, Upanga, upanga, hukumu, au turn it au njaa, tutasimama mbele ya nyumba hii na mbele zako,
(Maana Jina lako limo katika nyumba hii), na kukulilia katika shida yetu, Nawe utasikia na kuokoa.
Maana yake Nini?!
Mfalme yehoshafati alimlilia BWANA katika shida zao na kuiweka nyumba ya BWANA kuwa ndipo makimbilio yao Maana Jina lako limo ndani ya nyumba yako.
-Leo iweje nyumba ya BWANA ifungwe kwa sababu ya Covid-19 (Corona virus)
KANISA Ndiyo nguzo la Taifa,
Kamwe Covid-19 (Corona virus) haliwezi kulifunga kanisa Bali kanisa litaifunga Covid-19 (Corona virus) katika Jina la Yesu.
Amen.
By Bash*te B. Kado.
BCIM Ministries