Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo Kijenge

Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo Kijenge UKURASA HUU NI KWA AJILI YA MASUALA YA KANISA PEKEE HURUHUSIWI KUTUMA VITU AMBAVYO HAVIENDANI.

06/09/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA JUMATATU*

*JUMA LA ISHIRI LA ISHIRINI NA TATU MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*

*07 SEPTEMBA 2026*
*=≈========≈==*

*MASOMO YA MISA*

*SOMO LA KWANZA*

1Wakorintho,5:1-8
Habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe, nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, k**a vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

*Neno La Bwana.........*

*WIMBO WA KATIKATI*

Zaburi,5:4-6,11(K)8

1. Unawachukia wote watendao ubatili.
Utawaharibu wasemao uongo;
Bwana humzira mwuaji na mwenye hila.

*(K) Bwana, uniongoze kwa haki yako*

2. Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;
Mtu mwovu hatakaa kwako;
Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako.

*(K) Bwana, uniongoze kwa haki yako*

3. Nao wote wanaokukimbilia watafurahi;
Watapiga daima kelele za furaha.
Kwa kuwa Wewe unawahifadhi,
Walipendao jina lako watakufurahia.

*(K) Bwana, uniongoze kwa haki yako*

*SHANGILIO*

Zaburi,19:8

*Aleluya, Aleluya!*
Amri ya Bwana ni safi,
huyatia macho nuru.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

Luka,6:6-11

Ilikuwa siku ya sabato nyingine Yesu aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza. Na waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumsh*takia. Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama. Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza? Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu.

*Neno La Bwana......*

05/09/2026

*☘️TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA DOMINIKA☘️*

*☘️DOMINIKA YA ISHIRINI NA TATU MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA☘️*

*06 SEPTEMBA 2026*
*☘️=============☘️*

*☘️ANTIFONA YA KUINGIA☘️*

*Zaburi,119:137,124*

*☘️Ee Bwana, wewe ndiwe mwenye haki, na hukumu zako ni za adili. K**a zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako☘️*

*☘️☘️☘️☘️*
*KOLEKTA*
*☘️☘️☘️☘️*

*Ee Mungu, umetuletea ukombozi na kutufanya watoto wako. Utusikilize kwa wema sisi watoto wa upendo wako. Tunakuomba ili wote wanaomwamini Kristo wapewe uhuru wa kweli na urithi wa milele. Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu, milele na milele*

*☘️☘️☘️☘️☘️☘️☘️*
*MASOMO YA MISA*
*☘️☘️☘️☘️☘️☘️☘️*
*🎼🎼🎼🎼🎼🎼🎼*
*☘️☘️☘️☘️☘️☘️☘️*
*Ezekieli,.33:7-9*

*Zaburi,95:1-2,6-9, (K)7-8*

*Warumi,13:8-10*

*Yohane,14:23*

*Mathayo,18:15-20*
*☘️☘️☘️☘️☘️☘️☘️*
*🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶*
*☘️☘️☘️☘️☘️☘️☘️*

*SOMO LA KWANZA*

*Ezekieli,.33:7-9*

Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.

*Neno La Bwana..........*

*WIMBO WA KATIKATI*

*Zaburi,95:1-2,6-9, (K)7-8*

1. Njoni tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.

*(K) Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!Msifanye migumu mioyo yetu*

2. Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.

*(K) Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!Msifanye migumu mioyo yetu*

3. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msifanye migumu mioyo yenu;
K**a vile huko Meriba;
K**a siku ya Masa jangwani,
Hapo waliponijaribu baba zenu;
Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

*(K) Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!Msifanye migumu mioyo yetu*

*SOMO LA PILI*

*Warumi,13:8-10*

Ndugu zangu, msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani, na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako k**a nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya, basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

*Neno La Bwana.....*

*SHANGILIO*

*Yohane,14:23*

*Aleluya, Aleluya!*

Mtu akinipenda, atalishika neno langu,
Na Baba yangu atampenda;
Nasi tutakuja kwake.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

*Mathayo,18:15-20*

Siku ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, k**a hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie Kanisa; na asipolisikiliza Kanisa pia, na awe kwako k**a mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

*Neno La Bwana.........*

04/09/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA JUMAMOSI*

*JUMA LA ISHIRINI NA MBILI MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KAMISA*

*05 SEPTEMBA 2026*
*---------------‐'--------*

*MASOMO YA MISA*

*SOMO LA KWANZA*

1Wakorintho,4:6-15

Ndugu zangu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe. Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi! Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, k**a watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu. Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; kisha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; tukisingiziwa twasihi; tumefanywa k**a takataka za dunia, na tamaa ya vitu vyote hata sasa. Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya k**a watoto niwapendao. Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.

*Neno La Bwana.........*

*WIMBO WA KATIKATI*

Zaburi.145:17-21(K)18

1. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
Bwana yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu.

*(K) Bwana yu karibu na wote wamwitao*

2. Atawafanyia wamchao matakwa yao,
Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Bwana huwahifadhi wote wampendao,
Na wote wasio haki atawaangamiza.

*(K) Bwana yu karibu na wote wamwitao*

3. Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu
milele na milele.

*(K) Bwana yu karibu na wote wamwitao*

*SHANGILIO*

Zaburi,119:18

*Aleluya, Aleluya!*

Unifumbue macho yangu, niyatazame,
Maajabu yatokayo katika sheria yako.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

Luka,6:1-5

Ilikuwa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao. Basi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia, Mbona mnafanya lisilo halali siku ya sabato? Yesu akawajibu akawaambia, Hamkulisoma hata hilo alilolifanya Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wale aliokuwa nao? Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya Wonyesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao. Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

*Neno La Bwana.......*

03/09/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA IJUMAA*

*JUMA LA ISHIRINI NA MBILI MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*


*04 SEPTEMBA 2026*
*---------------------------*
*MASOMO YA MISA*

*SOMO: LA KWANZA*

1Wakorintho,.4:1-5
Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu. Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu. Maana sijui sababu ya kujish*taki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana. Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

*,Neno La Bwana.........*

*WIMBO WA KATIKATI:*

Zaburi,.37:3-6,27,28,39-40(K)39

1. Umkabizi Bwana njia yako,
Pia umtumaini, naye atafanya.
Atajitokeza haki yako k**a nuru,
Na hukumu yako k**a adhuhuri.

*(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana*

2. Umtumaini Bwana ukatende mema,
Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
Nawe utajifurahisha kwa Bwana,
Naye atakupa haja za moyo wako.

*(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana*

3. Jiepue na uovu, utende mema,
Na kukaa hata milele.
Kwa kuwa Bwana hupenda haki,
Wala hawaachi watauwa wake.

*(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana*

4. Na wokovu wa wenye haki una Bwana;
Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
Naye Bwana huwasaidia na kuwaopoa;
Huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa;
Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.

*(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana*

*SHANGILIO*

Zaburi,.25:4,5

*Aleluya, Aleluya!*

Ee Bwana, unijulishe njia zako,
unifundishe mapito yako.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

Luka,.5:33-39

Mafarisayo na waandishi walimwambia Yesu, Wanafunzi wa Yohane hufunga mara nyingi, na kuomba dua; na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo; lakini wanafunzi wako hula na kunywa! Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile. Akawaambia na mithali, Hakuna akataye kiraka cha vazi jipya na kukitia katika vazi kuukuu; na k**a akitia, amelikata lile jipya, na kile kiraka cha vazi jipya hakilingani na lile vazi kuukuu. Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; na k**a akitia, ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe itamwagika, na viriba vitaharibika. Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya. Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema.

*Neno La Bwana.......*

02/09/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA ALHAMISI*

*JUMA LA ISHIRINI NA MBILI MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*

*03 SEPTEMBA 2026*
* # # # # # # # # # # # # # # # # #*

*MASOMO YA MISA*

*SOMO LA KWANZA*

1Wakorintho,3:18-23

Mtu asijidanganye mwenyewe; k**a mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

*Neno La Bwana........*

*WIMBO WA KATIKATI*

Zaburi,24:1-6(K)1

1. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia na wote wakaao ndani yake.
Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.

*(K) Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana*

2. Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili,
Wala hakuapa kwa hila.

*(K) Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana*

3. Atapokea Baraka kwa Bwana,
Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

*(K) Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana*

*SHANGILIO*

1Wathesalonike,2:13

*Aleluya, Aleluya!*

Lipokeeni neno la Mungu,
siyo k**a neno la wanadamu,
bali k**a neno la Mungu.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

Luka,5:1-11
Makutano walipomsonga Yesu wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti, akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao. Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni. Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. Simony akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama. Simoni Petro alipona hayo, alianguka magotini pa yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki waliopata; na kadhalika Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu. Hata walipokwisha kuviegesha pwani vyombo vyao, wakaacha vyote wakamfuata.

*Neno La Bwana........*

01/09/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA JUMATANO*

*JUMA LA ISHIRINI NA MBILI MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*

*02 SEPTEMBA 2026*
*>>>>>*

*MASOMO YA MISA*

*MASOMO YA MISA*

*SOMO LA KWANZA*

1Wakorintho,.3:1-9

Ndugu zangu, mimi siwezi kusema nanyi k**a na watu wenye tabia ya rohoni, bali k**a na watu wenye tabia ya mwilini, k**a na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu k**a Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

*Neno La Bwana.......*

*WIMBO WA KATIKATI*

Zaburi,33:12-15,20-21(K)12

1. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia.

*(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake*

2. Toka mahali pake aketipo
Huwaangalia wote wakaao duniani.
Yeye aiumbaye mioyo yao wote
Huzifikiri kazi zao zote.

*(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake*

3. Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Maana mioyo yenu itamfurahia,
Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.

*(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake*

*SHANGILIO*

Yakobo,.1:21

*Aleluya, Aleluya!*

Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani,
liwezalo kuziokoa roho zenu.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

Luka,4:38-44
Yesu alitoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake. Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara hiyo akaondoka, akawatumikia. Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya. Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo. Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafuta-tafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao. Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.

*Neno La Bwana.......*

31/08/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA JUMANNE*

*JUMA LA ISHIRI NA MBILI MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*

*01 SEPTEMBA 2026*
*>*

*MASOMO YA MISA*

*SOMO LA KWANZA*

Wakorintho,.2:10-16

Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni kuyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

*Neno La Bwana.......*

*WIMBO WA KATIKATI*

Zaburi,145:8-14(K)17

1. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
Bwana ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.

*(K) Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote*

2. Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.

*(K) Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote*

3. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
Bwana huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini.

*(K) Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote*

*SHANGILIO*

Waebrania,4:12

*Aleluya, Aleluya!*

Neno la Mungu li hai tena li na nguvu,
li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

Luka,4:31-37

Yesu alishuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato; wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo. Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno. Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka. Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile.

*Neno La Bwana........*

30/08/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA JUMATATU*

*JUMA LA ISHIRINI NA MBILI MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*

*31 AGOSTI 2026*
*>>

29/08/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MISA YA DOMINIKA*

*DOMINIKA YA ISHIRINI NA MBILI MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*

*30 AGOSTI 2026*
*>*

*ANTIFONA YA KUINGIA*

*Zaburi,86:3,5*

*Wewe, Bwana, unifadhili, maana nakulilia wewe mchana kutwa. Kwa maana wewe, Bwana, u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao*

*KOLEKTA*

*Ee Mungu wa majeshi, ambaye kila kilicho bora ni chako, ututilie mioyoni mwetu upendo wa jina lako. Pia, kwa kutuongezea uchaji, uyasitawishe ndani yetu yale yaliyo mema, na uyahifadhi kwa ulinzi wako imara yale uliyoyasitawisha. Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu, milele na milele*
*🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶*
*MASOMO YA MISA*
*🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶*
*🎼🎼🎼🎼🎼🎼🎼🎼*
*🎹🎹🎹🎹🎹🎹🎹🎹*

*Yeremia,20:7-9*

*Zaburi,63:1-5,7-8,(K)1a*

*Warumi,12:1-2*

*Luka,.21:36*

*Mathayo,16:21-27*
*🎵🎵🎵🎵🎵🎵🎵*
*🎼🎼🎼🎼🎼🎼🎼*
*🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶*
*>>

28/08/2026

*TAFAKARI YA MASOMO YA MUSA YA JUMAMOSI*

*KIFODINI CHA MTAKATIFU YOHANE MBATIZAJI*

*JUMA LA ISHIRINI NA MOJA MWAKA A KIPINDI CHA KAWAIDA CHA KANISA*

*29 AGOSTI 2026*
*>>>>*

*MASOMO YA MISA*

*SOMO LA KWANZA*

Yeremia,1:17-19

Neno la Bwana lilinijia, Haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke, ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao. Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii. Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe.

*Neno La Bwana....*

*WIMBO WA KATIKATI*

Zaburi,71:1-6,15,17 (K)15

1. Nimekukimbilia Wewe, Bwana,
Nisiaibike milele.
Kwa haki yako uniponye, uniopoe,
Unitegee sikio lako, uniokoe.

*(K) Kinywa changu kitasimulia haki yako*

2. Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,
Nitakakokwenda siku zote.
Umeamuru niokolewe,
Ndiwe genge langu na ngome yangu.
Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi.

*(K) Kinywa changu kitasimulia haki yako*

3. Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana Mungu,
Tumaini langu tokea ujana wangu.
Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,
Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,
Ninakusifu Wewe daima.

*(K) Kinywa changu kitasimulia haki yako*

4. Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako,
Mchana kutwa; maana sijui hesabu yake.
Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu,
Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata milele.

*(K) Kinywa changu kitasimulia haki yako*

*SHANGILIO*

Mathayo.5:10

*Aleluya, Aleluya!*

Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki,
maana ufalme wa mbinguni ni wao.

*Aleluya!*

*SOMO LA INJILI*

Marko,6:17-29

Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, kumk**ata Yohane, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo ndugu yake; kwa kuwa amemwoa; kwa sababu Yohane alimwambia Herodi, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo. Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate. Maana Herodi alimwogopa Yohane; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana, naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha. Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya; ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalame akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakaloniomba nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu. Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mfalme akafanya huzuni sana lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia. Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi, akaenda, akamkata kichwa mle gerezani, akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye. Wanafunzi wake waliposikia habari, walikwenda wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.

*Neno La Bwana........*

Address

Kijenge Box 3071
Arusha
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo Kijenge posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share