ELCT Diocese of Meru

ELCT Diocese of Meru "KAZI YA MUNGU,MIKONO YETU"

24/08/2026

BREAKING NEWS

Msaidizi wa Askofu aliyechaguliwa hivi punde na Mkutano Mkuu wa 17 wa KKKT Dayosisi ya Meru ni Mchungaji Abel Sawe Kaaya.

Atakuwa Msaidizi wa Askofu Mteule hadi atakapoingizwa kazini.

24/08/2026

BREAKING NEWS.

Rasmi Mkutano Mkuu wa 17 wa KKKT Dayosisi ya Meru umemchagua Mchungaji Ndelekwa Kuvavenaeli Pallangyo kuwa Askofu wa tatu wa Dayosisi.

Kwa sasa hadi kuingizwa kazini atakuwa Askofu Mteule.

Habari zaidi na picha ziinawajia

UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA 17 WA DAYOSISI.Ibada ya Siku ya Bwana leo tarehe 23/08/2026 iliambatana na ufunguzi wa Mkuta...
23/08/2026

UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA 17 WA DAYOSISI.

Ibada ya Siku ya Bwana leo tarehe 23/08/2026 iliambatana na ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 17 wa KKKT Dayosisi ya Meru. Mgeni rasmi katika Ibada ya ufunguzi wa Mkutano alikuwa Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa, Mkuu wa KKKT.

Mkutano utaendelea hadi tarehe 25/08/2026. Mkutano huu utakuwa na uchaguzi wa Askofu na Msaidizi wa Askofu. Maaskofu waliohudhuria Ibada ya ufunguzi wa Mkutano wamesisitiza umuhimu wa kumsikiliza Mungu anasema nini.

"KAZI YA MUNGU, MIKONO YETU"

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Dayosisi yakiwa kwenye hatua za mwisho. KARIBUNI WOTE
22/08/2026

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Dayosisi yakiwa kwenye hatua za mwisho.
KARIBUNI WOTE

Karibuni. Pia maombi yenu nì muhimu kufanikisha Mkutano
21/08/2026

Karibuni. Pia maombi yenu nì muhimu kufanikisha Mkutano

UZINDUZI WA OFISI YA USHARIKA - SONGOROKatika Siku ya Bwana ya 11 baada ya Utatu Usharika wa Songoro, lilifanyika pia te...
17/08/2026

UZINDUZI WA OFISI YA USHARIKA - SONGORO

Katika Siku ya Bwana ya 11 baada ya Utatu Usharika wa Songoro, lilifanyika pia tendo la baraka la uzinduzi wa Ofisi ya Usharika. Jengo la ofisi linajumuisha pia darasa la shule ya Jumapili. Ibada iliongozwa na Baba Askofu Elias K. Nasari, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Meru.

Baba Askofu aliwapongeza Washarika kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha huduma za Kanisa.

"KAZI YA MUNGU, MIKONO YETU"

MATENDO YA BARAKA - USHARIKA WA KILIMAMOJATarehe 13/08/2026 yalifanyika matendo ya baraka Usharika wa Kilimamoja. Matend...
14/08/2026

MATENDO YA BARAKA - USHARIKA WA KILIMAMOJA

Tarehe 13/08/2026 yalifanyika matendo ya baraka Usharika wa Kilimamoja. Matendo hayo ni kuwekwa wakfu kiwanja cha Mtaa mpya, kuwekwa jiwe la msingi Mtaa wa Penuel, kuzinduliwa jengo la shule ya Jumapili na kuzinduliwa rasmi Usharika wa Kilimamoja. Matendo yote hayo yalifanywa na Baba Askofu Elias K. Nasari, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Meru.

Baba Askofu aliwashukuru na kuwapongeza Wanakilimamoja kwa jinsi wanavyotekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Dayosisi "Kazi ya Mungu, Mikono yetu". Pia aliwaomba Washarika na Viongozi wa Serikali kutoa maeneo zaidi kwa ajili ya ukuaji wa Kanisa.

"KAZI YA MUNGU, MIKONO YETU"

Mwaliko kujiunga na Ailanga Lutheran Junior Seminary. USIKOSE
12/08/2026

Mwaliko kujiunga na Ailanga Lutheran Junior Seminary. USIKOSE

Karibuni Ngarenanyuki sekondari kwa elimu bora na malezi mazuri.
12/08/2026

Karibuni Ngarenanyuki sekondari kwa elimu bora na malezi mazuri.

KUZINDULIWA ENEO LA MTAATarehe 06/08/2026 Baba Askofu Elias Kitoi Nasari, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Meru aliweka wakfu ki...
07/08/2026

KUZINDULIWA ENEO LA MTAA

Tarehe 06/08/2026 Baba Askofu Elias Kitoi Nasari, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Meru aliweka wakfu kiwanja cha Mtaa mpya wa Nkiraansha uliopo Usharika wa Kitefu katika Ibada maalum. Tafsiri ya Kiswahili ya neno Nkira-ansha ni Mwokozi/Mponya amekuja.

Baba Askofu alieleza furaha yake kwa namna Kanisa linavyokua ikiwa ni mojawapo ya mipango ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Aliwahimiza Washarika kutafuta maeneo zaidi kwa ajili ya huduma inayozidi kukua. Washiriki wa Ibada walihamasika kuanza uchangiaji wa kuanza ujenzi wa jengo la Kuabudia ambapo zaidi ya Shilingi za Kitanzania milioni mbili na mabati vilipatikana.

"KAZI YA MUNGU, MIKONO YETU"

Address

Leganga
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ELCT Diocese of Meru posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share