EFatha Church Usariva- Arusha

EFatha Church Usariva- Arusha kanisa hili LENYE misingi yake mikuu ya kufungua maisha ya watu.Mark7:34

Kanisa la Efatha usariva Arusha, linapatikana kituo Cha Liganga, kwenye WILAYA ya Meru, Chini ya kiongozi mkuu wa makanisa ya Efatha Duniani Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

3. NYAKATI ZA KUMKUMBUSHA BWANAIsaya 66:6 “ Sauti ya fujo itokayo mjini! Sauti itokayo hekaluni! Sauti ya Bwana awalipay...
19/07/2026

3. NYAKATI ZA KUMKUMBUSHA BWANA

Isaya 66:6 “ Sauti ya fujo itokayo mjini! Sauti itokayo hekaluni! Sauti ya Bwana awalipaye adui zake adhabu!”

Nyakati za kumkumbusha Bwana kisiwe kipindi cha kukaa kimya bali roho mtakatifu akuongoze. Kwa nini usimwache Mungu akaye kimya? Bali unamkumbusha Bwana Yesu maana tunajua Yeye ni mpaji wa vyote, maana sisi tunamtegemea Yeye

Isaya 43:26 “Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.”

Mungu anasema umkumbushe ili aone uzingativu wako katika kukiri au kutangaza yale ambayo Mungu unatamani akuridhie ili akupe ahadi na baraka zake. Kipindi cha kumkumbusha Bwana ni kipindi cha kuumba nini kitokee.

Katika nyakati za kumkumbusha Bwana ni nyakati za ibada yaani hupaswi kukosa katika ibada na mikesha. Nyakati hizi shetani anapambana kung’oa waliookoka warudi duniani hivyo hizi ni nyakati za kumtafuta Mungu kweli kweli.

Isaya 62:6 “Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.

©KIONGOZI WA KIROHO WA KANISA LA EFATHA - MTUME NOEL KAPINGA

NENO LA SIKUNa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Kanisa la EfathaTarehe 13/07/2026SOMO: ILI UPOKEE YALE MUNGU ALI...
14/07/2026

NENO LA SIKU

Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Kanisa la Efatha

Tarehe 13/07/2026

SOMO: ILI UPOKEE YALE MUNGU ALIYOKUANDALIA ACHA KUWA NA IMANI HABA

Mathayo 14:31 “Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?” Hii inamaana kuwa Yesu alimuuliza kwa nini unamashaka, hata sasa anakuuliza wewe kwa nini una mashaka? Kitabu hiki kinafunua tabia ya imani.

Katika Biblia kuna aina tatu za wenye Imani,
1. Imani kubwa
2. Imani ndogo
3. Kutokuwa na imani kabisa (imani haba)

Mashaka ni tunda la hofu, palipo na hofu kuna mashaka nyingi, hofu hutokana na matukio, matukio yanapotokea yanaweza kuleta hofu inayosababishwa na yale yanayotokea katika mazingira yako.
Matukio yanatokea katika maisha yako na yanakujengea hofu na hiyo hofu inazalisha mashaka. Unakuwa na hofu juu ya kitu fulani kwa sababu ya tukio fulani lililotokea kwenye maisha yako na ndipo unaanza kuwa na mashaka.

Yesu aliwaamuru wanafunzi waingie kwenye chombo na watangulie mbele yake, pasipo Yeye kwenda nao, walipokuwa katikati ya bahari mawimbi na upepo ukaja, ndipo Yesu akaja kwao akitembea juu ya maji ili kutuliza dhoruba ndipo wanafunzi wake wakawa na mashaka k**a kweli ni Yesu.

Yesu anaweza kuja kwako katika namna ambayo si ya kawaida na wewe ukawa na mashaka na hofu hivyo ukashindwa kupokea yale ambayo Mungu amekukusudia katika maisha yako, hivyo ili uweze kupokea yale uliyokusudiwa jifunze kuwa na Imani wakati wote.

13/07/2026
13/07/2026

MUNGU NDIYE ANAYEJUA SAFARI YAKO
Follow for more

12/07/2026

Sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana" kutoka kwenye Zaburi 118:17, inayoeleza tumaini la kuishi na ushindi dhidi ya kifo. Kwamba aliyeokoka Hafariki Bali ufa kwa maana ya kulala na baadae uamshwa na kuchukuliwa kwenda nyumbani Mbinguni, Bali anayefariki ni yule ambaye upelekewa kwenda kusubiria ukumu ya umelele ya Jehanamu.
na Nabii Josephat Eliasi Mwingira.
Leo tarehe 12th July 2026.

02/07/2026

*⛪ KANISA LA EFATHA USARIVA – ARUSHA*
_Linakuletea_

*"MBEGU YA MAARIFA, MZIZI WAKE NI MUNGU"*
_Ibada na Kuwekwa Wakfu_
_kwa Wazazi na Wanafunzi Wote Wanaorudi Shule_

---

*✨ KAULI MBIU:*
_"Shule ni mbegu, lakini Mungu ndiye mzizi"_

*📖 NENO LA BWANA:*
_Danieli 1:17_ – _“Kwa vijana hao wanne, Mungu aliwapa maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandishi na hekima.”_

---

*📅 TAREHE:* Ijumaa, 3 Julai 2026
*🕒 MUDA:* Saa 9:00 Alasiri
*👨‍👩‍👧‍👦 WALENGWA:* Wazazi wenye watoto + Wanafunzi wote

* *

*⛪ KANISA LA EFATHA USARIVA – ARUSHA*  _Linakuletea_ *"MBEGU YA MAARIFA, MZIZI WAKE NI MUNGU"* _Ibada na Kuwekwa Wakfu_ ...
02/07/2026

*⛪ KANISA LA EFATHA USARIVA – ARUSHA*
_Linakuletea_

*"MBEGU YA MAARIFA, MZIZI WAKE NI MUNGU"*
_Ibada na Kuwekwa Wakfu_
_kwa Wazazi na Wanafunzi Wote Wanaorudi Shule_

---

*✨ KAULI MBIU:*
_"Shule ni mbegu, lakini Mungu ndiye mzizi"_

*📖 NENO LA BWANA:*
_Danieli 1:17_ – _“Kwa vijana hao wanne, Mungu aliwapa maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandishi na hekima.”_

---

*📅 TAREHE:* Ijumaa, 3 Julai 2026
*🕒 MUDA:* Saa 9:00 Alasiri
*👨‍👩‍👧‍👦 WALENGWA:* Wazazi wenye watoto + Wanafunzi wote

Address

S. L. P 42726
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EFatha Church Usariva- Arusha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share