02/10/2020
... 1 Wakorintho 1:25-29..Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu, bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu, tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, Amen! Hakuna anayeweza kuelezea vile Mungu hufanya kazi, yeye anachukua kitu dhaifu, kitu kinyonge anakifanya cha dhamana. Amewaaibisha na kunyamazisha waliodhania Wana nguvu Sana mbele ya Wale wanaooneka kuwa wanyonge, ili pasiwe na wa kujigamba mbele zake. Mwezi huu wa Oktoba, wacha Mungu aaibishe waliodhania Wana nguvu Sana na ainue wanyonge na vitu dhaifu. Uwe na wikendi tulivu majaliwa tuonane Jumapili tupeperushe bendera ya 5am -10am. Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili