03/04/2026
IBADA YA MKESHA WA PASAKA
SOMO: NGUVU YA WOKOVU KATIKA MSALABA
MUHUBIRI: Bishop Solomon Neema
UTANGULIZI
Msalaba wa yesu ni ishara ya mizigo ya dhambi na vifungo pamoja Na hukumu ya wanadamu.
Mathayo 2:13-15
Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.
Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;
Akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema,
Kutoka Misri nalimwita mwanangu.
Marko 15:25-32
Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.
Palikuwa na anwani ya mash*taka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.
Na pamoja naye walisulibisha wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.
Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa, wakisema, Ahaa! Wewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga katika siku tatu,
jiponye nafsi yako, ushuke msalabani.
Kadhalika na wakuu wa makuhani wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliponya wengine; hawezi kujiponya mwenyewe.
Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulibiwa pamoja naye wakamfyolea.
YESU ALIKUJA ILI SISI TUPATE NGUVU.
Lupita Kwa msalaba yesu aliwaleta wanadamu karibu Na Mungu. Mfalme Herode aliposkia habari za YESU was Nazareth alianza kupanic.
Usishangae Kwa nini watu wakikiona wanaanza kuleta ugomvi. Neema ya Mungu ina kanuni YA kuvutia upinzani. Hata wakikupinga hawatakuweza.
Mafarisayo Na masadukayo waliinuka Kwa ajili ya kumponga Kristo hata wakamuua. Hawakujia kumbe kufa Kwake ndio Faida kwetu. Alipokufa yesu mmoja, Wana wengine walizaliwa. Hao Wana ndio Mimi Na wewe. Yesu aliamua kufauta mapenzi YA baba yake akaja Duniani.
Aliamua kuishi chini ya Mamlaka ya neno la Mungu. Watu wengi wanapokuwa Na changamoto huwa zinawapndoa Katika nafasi.
YESU alikuwa anaweka malengo ya anafanya Bidii kuyatimiza malengo yake.
Kutembea Katika mwili.
Kufanya miujiza
Kufungua wafu
Kuwafungua waliofungwa.
Wewe uko Na malengo gani. YESU alikuwa amepanga hata namna ya kutoka Katika mtego wa Mauti.
Nitalivunja hekalu Kwa siku moja Na litalijenga Kwa siku tatu. Akijua manabii walisema nini juu yake. Naamuru KWA Jina la yesu.
Jamii yako ipone
Watoto wapone
Kazi yako iinuke.
NGUVU YA MSALABA NI GANI?
1. MSAMAHA WA DHAMBI KWA NJIA YA DAMU YA YESU WAEFESO 4:7
2. UHURU KUTOKA KWA LAANA ZOTE WAGALATIA 3:13
3.