06/02/2026
Kuacha uraibu ni sehemu ya maandalizi ya Ramadhani
Miongoni mwa maandalizi muhimu ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kutia nia ya dhati ya kuacha uraibu unaomchafua mwili na roho, k**a vile sigara, marungi, tumbaku na tabia nyingine zinazomchukiza Mwenyezi Mungu na kumdhuru mwanadamu.
Ramadhani ni mwezi wa kujizoesha subira na kujidhibiti. Mfungaji huacha chakula na kinywaji halali kwa ajili ya Allah, basi anaweza pia kuacha vilivyo haramu na vyenye madhara. Kuacha uraibu si jambo rahisi, lakini nia njema na msaada wa Mwenyezi Mungu humfanya jambo gumu liwezekane.
Anayeanza kabla ya Ramadhani huingia katika mwezi huu akiwa tayari zaidi, na anayechukua Ramadhani k**a fursa, anaweza kuufanya uwe mwanzo wa maisha mapya yaliyo safi na yenye afya.
Ramadhani ni mwezi wa mabadiliko โ anza leo.