24/06/2023
*MASOMO YA KILA SIKU*
*JUNI 23, 2023; IJUMAA:*
*JUMA LA 11 LA MWAKA*
*Mt. Yosefu Kafaso, Padre*
*SOMO 1:*
*2 Kor 11:18, 21-30*
Wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili, mimi nami nitajisifu. Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri. Wao ni Waebrania? Na mimi pia. Wao ni Waisraeli? Na mimi pia wao ni, uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia. Wao ni wahudumu wa Kristo? Nanena kiwazimu, mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote. Ni nani aliyedhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe? Ikinibidi kujisifu, nitajisifu mambo ya udhaifu wangu.
*WIMBO WA KATIKATI:*
*Zab. 34:1-6*
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
(K)Wenye haki Bwana anawaponya na taabu zao zote.
Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta Bwana akanijibu,
Akaniponya na hofu zangu zote. (K)
Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona haya.
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote. (K)
*INJILI:*
*Mt 6:19-23*
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo na wevi huvunja na kuiba;