17/11/2025
1 Wakorintho 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,
⁵ ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
⁶ Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
⁷ bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
⁸ ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana k**a wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;