LANGO La chemichemi

LANGO La chemichemi NAKUKARIBISHA KATIKA KUYATAFAKARI MAANDIKO.

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.                  MATHAYO 6:33
30/06/2025

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
MATHAYO 6:33

Je! Amri kuu ni ipi?Amri zote kumi za Mungu kiuharisia ziko sahihi lakini ukizifuata kisheria zitakutia udini tuLengo ku...
25/07/2022

Je! Amri kuu ni ipi?

Amri zote kumi za Mungu kiuharisia ziko sahihi lakini ukizifuata kisheria zitakutia udini tu

Lengo kuu la Mungu ilikuwa ni kukombolewa kupitia amri hizi, amri zote za Mungu hufanyika rohoni tofauti na torati ukweli ni kwamba amri za Mungu ni nyingi Sana, lakini torati Mungu aliweka amri kuu kumi. Vipi hapo? Je, ni haki kushika amri kuu kumi tu? Hasha! hiwezi kuwa hivyo.
Nasema amri za Mungu ni nyingi tu kwamfano, kuna amri za talaka, kutoa zaka, kuhusu sadaka, utoaji, kusaidia yatima, wajane na maskini, kuhusu kufunga, kuhusu kuua, kunyanganya, uzinzi, viapo na kadhalika
Mpendwa unaonaje ukizifuata amri kumi tu na kuziacha zingine zote, mpendwa ukizifuata kwa muongozo wa Sheria hakika utaanguka maana biblia inasema katika kitabu cha wagalatia 3:10 Kwa maana wale wote walio wa matendo ya Sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yalioandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye) soma WAEBRANIA 8:8-10 soma...

Basi amri kuu ni hii UPENDO na Yesu mwenyewe alisema katika mathayo 22:35-40 .35 mmoja wao, mwana sheria akamwuliza, akimjaribu. 36 mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?.37 Akamwambia , mpende Bwana Mungu wako Kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 HII NDIYO AMRI ILIYO KUU TENA NI YA KWANZA 39 Na ya pili ya, yafanana nayo, nayo ni hii mpende jirani yako k**a nafsi yako. 40 katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii

UPENDO huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari, upendo haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu , hauhesabu mabaya , haufurahii udhalimu, Bali hufurahi pamoja na kweli, upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, palipo upendo hapana chuki, hapana wivu, hapana hasira, hapana vita, hapana uchawi, hapana masengenyo,hapana uadui, hapana ugomvi, hapana ukabira, hapana tamaa, hapana kujipenda, hapana kutelekezwa, hapana kesi,hapana uchoyo....

Nikihitimisha Yesu anasema katika kitabu cha YOHANA 14:15 mkinipenda, mtazishika amri zangu.

Mpendwa siri ni Yesu Kristo pekee mjue leo Kwa kutubu na kumaanisha kuziacha dhabi zako zote , kisha tafuta ubatizo sahihi, ambao ni ule wamaji tele na kwa jina la Yesu Kristo, na kujiunga na kanisa sahihi linalo ongozwa na Roho mtakatifu.

Yesu amekuja kwetu kupitia Kwa Maria, basi twalazimika pia kwenda Kwa Yesu kupitia Maria huyohuyo.           Maneno hayo...
18/07/2022

Yesu amekuja kwetu kupitia Kwa Maria, basi twalazimika pia kwenda Kwa Yesu kupitia Maria huyohuyo.

Maneno hayo nmeyanukuu hapo juu☝️sio sahihi na nimafundisho mapotofu

Biblia inasema katika kitabu cha Hosea 4:6 watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
Kumbe silaha ya adui ni kumshambulia mtu na kumpoteza hasa yule asiye na ujuzi wa maandiko!
Madhehebu yaliyoko hapa duniani siku ya leo mengi yanafundisha mafundisho ya uongo. Mafundisho yasio mpa Yesu nafasi ya Kwanza ndani ya mioyo yetu.hakika ni mafundisho potofu

Namaanisha nini mpendwa? Fundisho lolote linalokuaminisha kuwa maria ni muombezi wetu, basi ujue ni fundisho la kupotosha epukana nalo. YOHANA 14:6 Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima: mtu haji Kwa Baba, ila Kwa njia ya Mimi.
Huu ni mstari☝️kutoka katika kitabu kitakatifu cha Mungu ukielezea waziwazi yakuwa hakuna njia ya kwenda Kwa Baba wala hakuna kweli ingine ijapokuwa Yesu Kristo pekee
Biblia inasema katika kitabu cha WAEBRANIA 4:12 yakwamba neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena linaukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena la choma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Je! maria ninani kimaandiko? maria ni mbarikiwa wala simtakatifu tunashuhudia maria akijielezea kuwa yeye ni nani- tusome LUKA 1:46-49) 46. mariamu akasema, moyo wangu wamuadhimisha Bwana,
47. Na roho yangu imemfurahia Mungu, mwokozi wangu.
48. Kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake. KWAMAANA, TAZAMA, TOKEA, SASA VIZAZI VYOTE 👈 underline that; vizazi vyote WATANIITA MBARIKIWA;
49. Kwakuwa mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu.

Nikihitimisha fundisho la leo ndungu/dada mpendwa ni ushauri wangu kwako wewe ulie chini ya dini au mafundisho ya namna hiyo ya undanganyifu ukubali siku ya leo kujiunga na kanisa la kweli linalo ongozwa na Roho mtakatifu mkumbali Bwana wetu mwokozi Yesu Kristo kwa kuokoka nakumaanisha kisha ubatizwe ubatizo sahihi ambao ni kuzamishwa katika maji mengi YOHANA 3:23)

natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ame, Nakusihi mpokee Bwana maadamu anapatikana, yeye ndiye mlango pekee wakatu huu ulio wazi mlango wa neema. nak**a wewe ni mkristo jina au wewe ni mkristo vuguvugu mguu mmoja ndani ule mwingine inje nakusihi fanya maamuzi wakati huu

UFUNUO 3:16 basi, kwasababu Una uvuguvugu, wala hu baridi wala Moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

BWANA YESU AKUBARIKI! AMEEN

Hekima ya mwanadamu ni sawa na upumbavu mbele za Bwana, hivyo basi hekima ya mwanadamu haiwezi kuwaongoza watu kutenda h...
08/02/2022

Hekima ya mwanadamu ni sawa na upumbavu mbele za Bwana, hivyo basi hekima ya mwanadamu haiwezi kuwaongoza watu kutenda haki ya Mungu ! Omba kwamba Bwana akupe hekima ya kumjua yeye na kuwaongoza wengi kutenda! Lakini ikiwa wewe umezaliwa mara ya pili katika Bwana Yesu Tu!! Omba hekima Mpendwa.
1 WAKORINTHO 1:25
Upumbavu wa Mungu Una hekima zaindi ya mwanadamu, na udhaifu wa Mungu Una nguvu zaidi ya wanadamu.

1 Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako Kabla hazijaja siku zilizo mbaya wala haijakaribia miaka utakaposema mimi sina...
03/11/2021

1 Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako Kabla hazijaja siku zilizo mbaya wala haijakaribia miaka utakaposema mimi sina furaha katika hiyo.
2 Kabla jua na nuru na mwezi na nyota havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada mvua.
7 Nayo mavumbi kuirudia nchi k**a yalivyokuwa kuwa, na roho kumrudia Mungu aliyeitoa.

19/07/2021

Angalieni, kumtii Mungu ni bora kuliko kumtolea dhabihu, Na kumskia kuliko mafuta ya beberu.

Kutahiriwa na kutotahiriwa Hakuna maana, cha msingi ni kuutunza Moyo wako vizuri.MATENDO YA MITUME 11:2 Na petro alipopa...
19/07/2021

Kutahiriwa na kutotahiriwa Hakuna maana, cha msingi ni kuutunza Moyo wako vizuri.

MATENDO YA MITUME 11:2 Na petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye,

3 Wakisema, uliingia kwa watu wasio tahiriwa ukala nao.

4 Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema

5 Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba roho yangu ikazimia nikaona maono chombo kinashuka, k**a nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia

6 Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.

7 Nikaskia na sauti ikiniambia, ondoka, petro, ukachinje ule.

8 Nikasema, Hasha, Bwana, Kwa maana kitu kilicho au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu.

9 Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi.

Mpendwa sote tumekubarika
machoni pa Bwana

YAKOBO 3:3- Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.4 Tena angalieni...
19/07/2021

YAKOBO 3:3- Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.

4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa k**a nini, nakuchukuliwa na pepo Kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha

5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kindogo,nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uashavyo msitu mkubwa sana.

6 Nao ulimi ni Moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote najisi, huuwasha Moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanam.

7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na yavitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

8 Basi ulimi hakuna awezaye kuufuga; Ni uovu usiotulia, umekaa sumu iletayo mauti.


(((((MARKO 7:1- Kisha mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake,

2 Wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula Kwa mikono najisi, yaani, isiyo nawiwa.

3 Kwa maana mafarisayo na wayahudi wote wasipo nawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao;

4 tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; Nayako mambo mengine waliyopokea kuyashika, k**a kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.

5 Basi wale mafarisayo na waandishi wakamwuliza, mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, Bali hula chakula kwa mikono najisi?

14 Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu.

15 Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, Bali vile vimtokavyo mtu, ndivyo vimtiavyo unaji yule mtu.

18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;

19 Kwasababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.

20 Akasema, kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.

21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22 wivi, uuaji, usinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

TWENDENI GEREZANI TUKAWAELEWESHE ILI WATOKE NDANIFidia imelipwa tayari, Milango ya gereza ipo wazi lakini cha ajabu wasi...
26/05/2021

TWENDENI GEREZANI TUKAWAELEWESHE ILI WATOKE NDANI

Fidia imelipwa tayari, Milango ya gereza ipo wazi lakini cha ajabu wasio watumwa tena watumikishwa

JE! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini k**a ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia 1WAKORINTHO 7:21

ZABURI 92:12 Mwenye haki atasitawi k**a mtende, Atakuwa k**a mwerezi wa lebanoniZABURI 58:10 Mwenye haki atafurahi akion...
26/05/2021

ZABURI 92:12 Mwenye haki atasitawi k**a mtende, Atakuwa k**a mwerezi wa lebanoni
ZABURI 58:10 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi; Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki
ZABURI 64:10 Mwenye haki atamfurahia Bwana nakumkimbilia.

MWENYE HAKI ATAKUMBUKWA
MILELE

HOW BEAUTIFUL ARE THE FEET OF THEM THAT PREACH TRUE GOSPEL OF PEACE. NI MIZURI K**A NINI MIGUU YAO WAHUBIRIO HABARI YA M...
13/05/2021

HOW BEAUTIFUL ARE THE FEET OF THEM THAT PREACH TRUE GOSPEL OF PEACE. NI MIZURI K**A NINI MIGUU YAO WAHUBIRIO HABARI YA MEMA!

Address

Kiu River
Kahawa

Telephone

+254735935497

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LANGO La chemichemi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to LANGO La chemichemi:

Share