10/07/2026
Unaweza kuwaficha watu hisia zako, Unaweza kutabasamu wakati umeumia, Unaweza kusema "niko sawa" ilhali moyo wako umejaa maumivu, Lakini mbele za Mungu hakuna kinachofichika.
Mungu anajua kila kilicho moyoni mwako, Anajua machozi ambayo hayajaonekana, majeraha usiyoyasema na vita unavyopitia kimya kimya. Ndiyo maana hatuitwi kwenda mbele zake tukiwa na sura ya kujifanya, bali tukiwa na moyo wa kweli.
Karibu kujifunza kuhusu moja ya sifa za asili za Mungu Mungu Anajua Yote. Ujumbe huu utakusaidia kuelewa kwa nini uwazi mbele za Mungu ni mwanzo wa uponyaji na uhusiano wa karibu zaidi na Yeye.
Tazama mahubiri kamili, shiriki na mtu mwingine ambaye anahitaji kukumbushwa kwamba Mungu anamjua na anamhitaji aje mbele Zake jinsi alivyo.