13/08/2026
๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐
๐๐๐๐๐๐ :
Uongozi si nafasi ya heshima tu; ni nafasi ya kubeba uzito wa wengine.
Watu wengi wanapenda mamlaka ya uongozi, lakini hawataki gharama ya uongozi.
Biblia na viongozi wakubwa k**a Myles Munroe wanaonyesha kwamba kila kiongozi wa kweli anapitia majaribu yanayofanana.
Haijalishi unaongoza kanisa, taasisi, biashara, familia, shule au serikali, kuna mambo ambayo hutayaepuka.
1๏ธโฃ LAWAMA
Kiongozi ndiye mtu wa kwanza kulaumiwa mambo yanapoharibika, hata k**a chanzo cha tatizo hakikuwa yeye.
Israeli walimlaumu Musa karibu kila walipopitia changamoto. W
alimlaumu walipokosa maji, walipokosa chakula, walipoona maadui na hata walipochoshwa na safari ya jangwani (K*t. 15:24; 16:2-3; 17:2-3; Hes. 14:2).
Hivi ndivyo uongozi ulivyo. Mafanikio yakitokea wengi watasema "tulifanya," lakini matatizo yakitokea watasema "ulifanya."
Kiongozi lazima ajifunze kubeba lawama bila kupoteza maono.
---
2๏ธโฃ KUBEBA MATATIZO YA WALE UNAOWAONGOZA
Makosa ya unaowaongoza mara nyingi yatageuka kuwa mzigo wako.
Musa alilalamika mara kadhaa kwamba wana wa Israeli ndio waliomsababishia huzuni na adhabu ya kutokuingia Kanaani.
Soma:
- Kumbukumbu la Torati 1:37
- Kumbukumbu la Torati 3:26
- Kumbukumbu la Torati 4:21
Katika maandiko haya Musa anaonyesha kuwa kwa sababu ya watu aliokuwa akiwaongoza, walimsababishia matokeo makubwa kwenye maisha yake.
Kiongozi huwa anabeba uzito wa watu wake.
---
3๏ธโฃ KUSALITIWA
Hakuna uongozi usio na wasaliti.
Yesu alikuwa na wanafunzi kumi na wawili lakini mmoja wao akamsaliti.
Cha kushangaza ni kwamba usaliti mwingi hauji kutoka kwa maadui wa mbali bali kutoka kwa watu wa karibu.
Yuda hakumsaliti Yesu kwa kumpiga, bali kwa kumbusu.
(Mt. 26:47-50)
Kiongozi mwenye hekima hajifunzi kutokusalitiwa; anajifunza namna ya kuendelea mbele baada ya kusalitiwa.
---
4๏ธโฃ KUACHWA PEKE YAKO
Kiongozi mara nyingi huwa anabaki peke