Mungu ni mwema Fahamu mafumbo ya Mungu

29/09/2025

🌸Urembo wa kweli huanzia ndani.
Moyo mtakatifu, mawazo mema, na matendo mazuri huangaza zaidi kuliko muonekano wa nje.
Jilinde, jiheshimu, na uishi kwa wema kila siku.
Evangelist Dan Mott

05/04/2025
Watu wa Mungu tusichoke kumwomba huyu Mungu maana ndo msaada pekee wa karibu kwenye maisha yetu Wakati wengine wanataja ...
21/08/2024

Watu wa Mungu tusichoke kumwomba huyu Mungu maana ndo msaada pekee wa karibu kwenye maisha yetu

Wakati wengine wanataja magari, wakati wengine wanataja farasi, wakati wengine wanataja misaada ya kibinadamu waliyonayo, Sisi Acha tulitaje jina la Bwana wa Majeshi

Ninakuombea Jina Mungu wa Yakobo likuinue

Shetani akitaka usifanikishe baadhi ya maono yako. Atampiga kwanza mbeba majukumu ya familia yako.Jifunze kuombea famili...
16/08/2024

Shetani akitaka usifanikishe baadhi ya maono yako. Atampiga kwanza mbeba majukumu ya familia yako.

Jifunze kuombea familia yako yote

SHALOM ! MWANAFUNZI TULIYE ONGEA NAYE ALINIULIZA HIVI;Naomba unipe masomo ya kiroho na sheria za kimungu ili niweze kuis...
15/08/2024

SHALOM ! MWANAFUNZI TULIYE ONGEA NAYE ALINIULIZA HIVI;

Naomba unipe masomo ya kiroho na sheria za kimungu ili niweze kuishi maisha ya haki mbele za Mungu. Nataka kujua jinsi ya kumpendeza Mungu na kuishi maisha yanayompendeza.

Nimefurahi sana kukuona tena, mwalimu wangu. Natumai uko salama na unaendelea vizuri.

Mimi pia nimefurahi kukuona tena. Ninashukuru kwamba Mungu ametupa fursa nyingine ya kuongea pamoja.

Leo, nataka tuongelee kuhusu masomo ya kiroho na sheria za kimungu. Nataka kujifunza jinsi ya kumpendeza Mungu na kuishi maisha yanayompendeza.

Mimi niko tayari kukusaidia na hilo.

Masomo ya Kiroho

Masomo ya kiroho ni muhimu sana kwa Wakristo wote. Yanatusaidia kukua katika imani yetu na kumjua Mungu vizuri zaidi. Pia yanatusaidia kuishi maisha yanayompendeza.

Kuna masomo mengi tofauti ya kiroho ambayo tunaweza kujifunza. Baadhi ya masomo muhimu ni pamoja na:

* Upendo wa Mungu
* Neema ya Mungu
* Msamaha wa Mungu
* Utakatifu wa Mungu
* Utii wa Mungu

Sheria za Kimungu

Sheria za kimungu ni maagizo ambayo Mungu ametupa ili tuishi maisha yanayompendeza. Sheria hizi zinatusaidia kuepuka dhambi na kuishi maisha matakatifu.

Kuna sheria nyingi tofauti za kimungu. Baadhi ya sheria muhimu ni pamoja na:

* Amri Kumi
* Sheria ya Upendo
* Sheria ya Dhahabu

Jinsi ya Kumpendeza Mungu

Kuna mambo mengi tofauti ambayo tunaweza kufanya ili kumpendeza Mungu. Baadhi ya mambo muhimu ni pamoja na:

* Kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, roho yako yote, na akili yako yote.
* Kumpenda jirani yako k**a unavyojipenda mwenyewe.
* Kutii sheria za Mungu.
* Kuishi maisha matakatifu.
* Kueneza injili.

Jinsi ya Kuishi Maisha Yanayompendeza Mungu

Kuna mambo mengi tofauti ambayo tunaweza kufanya ili kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Baadhi ya mambo muhimu ni pamoja na:

* Kuomba kila siku.
* Kusoma Biblia kila siku.
* Kwenda kanisani kila Jumapili.
* Kutumikia wengine.
* Kuwa shahidi wa imani yako.

MUNGU AWABARIKI

KITABU HIKI KIPO DISPONIBLE KWENYE LUGHA YA KISWAHILI
06/08/2024

KITABU HIKI KIPO DISPONIBLE KWENYE LUGHA YA KISWAHILI

Mwanaume mmoja tajiri alienda kanisani akapiga magoti na kuanza kuomba akisema,,Ee Mungu hata lini nitateseka katika mag...
20/07/2024

Mwanaume mmoja tajiri alienda kanisani akapiga magoti na kuanza kuomba akisema,,Ee Mungu hata lini nitateseka katika magonjwa,nimekuwa mtu wa kuumwa kila siku, mwili wangu umekuwa makao ya kila Aina ya ugonjwa ukitoka ugonjwa huu unaingia ugonjwa mwingine Ee Mungu naomba uniponye

Wakati tajiri yule akiwa amepiga magoti anaomba pembeni yake kulikuwa na mwanaume mwingine maskini naye alikuwa akiomba tena kwa sauti kubwa ikiambatana na machozi

Maskini Aliomba Akisema,,Ee Mungu hata lini nitaendelea kuishi maisha haya ya Kimaskini angalia deni la kodi ya nyumba limekuwa kubwa sana Na mwenye nyumba amenipa siku chache na zikipita atanifukuza , Naomba Mungu usiache niaibike

Wakati maskini anaomba kwa sauti kubwa sana, Tajiri aliona maskini anampigia Kelele hivyo akamgusa na kumuuliza kwani Unadaiwa kodi ya Nyumba Tshs ngapi?... Mwanaume maskini akasema ni Tshs 100000{Laki moja} tajiri akamwambia nitakupatia 1000000{Milioni 1} Maskini alifurahi sana Na kuanza kumtukuza Mungu.

Nami nakutamkia kwamba Mungu atatumia watu ambao hukuwadhania kukupatia msaada na kukufikisha kwenye Hatima yako na ndivyo itakavyokuwa katika Jina la Yesu Kristo

Andika Amen naiwe kwako

22/03/2024

Hii ni kwa ajili ya Mwanamke ambae hajawahi kutembea na mume wa mtu au kuvunja ndoa ya mtu, Mungu akupe Mume muaminifu.

14/02/2024

Upendo na Udumu Milele. Somo la Kitabu cha Wimbo Ulio Bora umekuja wakati mwafaka kweli. 😂😂😂

Hebu tuombe pamoja sala ya afya na uponyaji kwa wale wanaougua na wenye mahitaji ya uponyaji:Ee Mungu mwenye nguvu na mw...
26/01/2024

Hebu tuombe pamoja sala ya afya na uponyaji kwa wale wanaougua na wenye mahitaji ya uponyaji:

Ee Mungu mwenye nguvu na mwenye huruma,
Tunakujia leo kuomba kwa niaba ya wote wanaougua na wenye mahitaji ya uponyaji.
Tunakuomba utazame kwa huruma juu ya wote wanaoteseka na magonjwa, maumivu, na udhaifu wa miili yao.

Tunakuomba utume uponyaji wako kwa miili yao na roho zao.
Mponye wagonjwa wetu kutoka kwa magonjwa yao yote, iwe ya kimwili, kiakili, au kiroho.
Wapatie faraja na ahueni kutoka kwa maumivu na mateso yao.

Ee Mungu mwenye hekima na mwenye ufahamu,
Tunakuomba utie uwezo katika mikono ya wafanyakazi wa afya na watoaji huduma.
Wabariki na kuwapa hekima, ujuzi, na uongozi wa kuponya wagonjwa kwa njia bora na yenye upendo.

Tunakuomba uponyaji wa haraka kwa wale walioko hospitalini na vitanda vya wagonjwa.
Wape nguvu na afya ili waweze kupona na kujiinua tena.
Wafariji na kuwapa matumaini wale wanaosubiri matibabu na uchunguzi.

Ee Mungu mwenye upendo na mwenye rehema,
Tunakuomba uwape faraja wale wanaowasaidia wagonjwa na kuwatunza.
Wape ustahimilivu na nguvu ya kusaidia na kutunza wapendwa wao.

Tunakuomba utupe sisi sote moyo wa kuwajali na kuwasaidia wagonjwa na wale wanaoteseka.
Tuongoze kuwa watu wenye huruma na wenye uelewa, tayari kusaidia wengine katika nyakati za mahitaji.

Tunakuomba utuletee afya na uponyaji katika ulimwengu huu wenye mahitaji mengi.
Tupe afya njema ya mwili, akili, na roho ili tuweze kutumika katika huduma yako.

Tunakushukuru, Ee Mungu, kwa kusikia sala zetu na kutujibu kwa mapenzi yako mema.
Tunakushukuru kwa baraka zako na uponyaji wako.
Tunatuma sala hii kupitia jina lako takatifu. Amina.

WEWE YONA! NINAWI UTAKWENDA AU UTAKIMBILIA TARSHISHI?Kila mmoja wetu anao wito maalum tofauti na mwenzake hapa duniani; ...
24/01/2024

WEWE YONA!
NINAWI UTAKWENDA AU UTAKIMBILIA TARSHISHI?

Kila mmoja wetu anao wito maalum tofauti na mwenzake hapa duniani; huyu hivi na yule vile. Huyu anatumwa NINAWI anaenda TARSHISHI kwa sababu kaona watu wengine wanaenda huko!

Tatizo la watu wengi kuishi kwenye matatizo, changamoto na shida zisizo koma au kukosa raha na furaha ya maisha hata k**a wana pesa, ni kwa sababu ya kuacha miito yao au makusudi ya wao kuja duniani na kukimbizana na majukumu ya watu wengine. Hili ni tatizo kubwa sana hususani hapa Afrika; watu wako kwenye Ofisi si zao. Ni kina Yona, yule wa kwenye Biblia. Wito wake ni kwenda NINAWI kuhubiri toba, yeye anakimbilia kwenye meli ya wafanyabishara kwenda TARSHISHI!

Baba ambaye anakimbia wito wake atatesa sana familia yake, mkewe na watoto wataishi kwenye shida, taabu na mateso kupita kawaida!

Mchungaji mmoja alinipigia simu kwa huzuni akiniambia "Mtu wa Mungu nisaidie mimi. Nina miaka 16 kwenye huduma mambo hayaendi kabisa, chakula shida na mahitaji mengine. Mke wangu kanikimbia, nisaidie, napitia majaribu makubwa sana. Nimefunga na kuomba, nimepakwa sana mafuta, lakini sioni mabadiliko, nataka niache huduma nirudi kijijini na familia maana hata umri unakwenda!"

Nilipokuja kumfuatilia kinyota nikagundua yeye ni 'born a leader' ambaye hakutakiwa kuwa muhubiri wa Injili Kanisani (Mchungaji) alitakiwa kuwa muhubiri wa Injili Serikalini na kwenye taasisi kwa sababu hatima yake na wito wake ulikuwa kufanya kazi za kiutawala!
Remember; Injili ni habari njema. Huyu pastor hakutakiwa kuwa Kanisani alitakiwa kuwa public figure kupitia Utawala Serikalini!
Ni Yona aliyeabiri meli kwenda TARSHISHI badala ya NINAWI!

Aliona wengine wanahubiri makanisani akapenda akaenda huko. Akakutana na Samaki mkubwa (nyangumi) akammeza!

Ndio maana anapitia yote anayoyapitia kwa miaka 16 mfurulizo kwenye kazi ya kichungaji!

Mwingine yuko Mbeya mjini.
Huyu alitakiwa kuwa Mwimbaji wa muziki akaenda kuanzisha Kanisa vijijini. Miaka zaidi ya 5 bila wafuasi!
Alipojitambua akabadili GIA angani akaanza kuimba Muziki wa Injili k**a basic call huku akichunga Kanisa.

Muda mchache baadaye akaanza kuona matokeo makubwa kupitia muziki. Akajenga, akanunua Prado, akajenga Kanisa lake, akapeleka watoto shule na wafuasi wakaanza kumfuata huko huko Kanisani kwake ili wasikilize nyimbo zake sio mahubiri wala mafundisho yake!

Truly, I tell you. Huyu Mchungaji Mwimbaji asingeshtuka, mpaka leo angekuwa pabaya sana. Life would have been very very hard and difficult.
Watu wengi ambao hawajashtuka, hawajajitambua, bado wanasota kwenye tumbo la nyangumi.
Wakijielewa nyangumi atawatapika, ili waende NINAWI kwenye wito wao.

Hakuna mtu anayeweza kutulia kwenye hii dunia bila kujua wito wake ni hupi. Wengi sana wanaangaika kutafuta pesa, hawapati na wanaopata wana presha, sukari, maradhi ya moyo na sonona, kwa sababu FEDHA SIO SULUHISHO kwa mtu aliyekumbia wito wake!

Mtu alitakiwa awe business man mzuri wa kusambaza maji mikoa mbalimbali na nje ya nchi, lakini cha ajabu yupo kwenye hema anaombea watu na kuwauzia maji!!!!
Ni Mfanyabishara aliyejivika joho la mtume au nabii!

A true prophet/ prophetess, never sell the so called 'spiritual commodities' ili apate hela. Wito wake haupo kwenye hela. Water selling prophets, oil selling apostles waacheni wanatafutia familia zao, sio wito wao ndio maana hawana raha pia.
Prophets of whom I know ni mountain men, ni watu wa faragha huko milimani; kula, kuvaa na kula bata town sio inshu zao hizo, nendeni mkafuatilie.

Nikisema hivyo utasikia watu wanang'aka "mbona tunapona?"

Mi sijasema hamponi, mnapona just because you believe!
Acha kuamini tuone k**a utapona!

Yote yawezekana kwake aaminiye. Wapo wanaopona kwa kwenda kwa waganga wakapiga manyanga na kuchezea tunguli wakaponywa.
Wapo wanaoponywa kwa kula mizizi, wengine kuchemsha majani ya miti fulani na wengine kwa kwenda hospitalini. Uongo???

Anyway, mada yetu ni YONA NA NINAWI, sio?

Tuendelee...

Ukigundua wito wako au kusudi lako la kuishi sio hicho unachojishughulisha nacho ujue umekosea, umeacha kwenda NINAWI umekimbilia TARSHISHI.
K**a huna raha na kazi yako hata k**a inakupa hela nzuri acha maana unapoteza muda, tafuta kujua kusudi lako maalum.

K**a unachofanya kinakupa amani, raha na furaha hata k**a hakikupi fedha nyingi komaa nacho maana ndio wito wako na mahitaji yako yote na ya familia yako yatapatikana humo humo.

Usiponielewa leo kesho ipo. Sio kila mtu ni fast learner. Wengine tuna vichwa ngumu, kuelewa haraka ni jaribu!

Somo litaendelea . . .

Ukitaka ushauri wowote wa masuala ya kiroho, inbox.!

Adresse

Masisi

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Mungu ni mwema publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Partager