28/06/2026
SOMO: ALAMA 7 ZA KURUDI KWA BWANA YESU KRISTO NA MIFANO TUNAYOONA LEO*
*Fungu kuu: Mathayo 24:33*
_"Nanyi kadhalika, mkiona hayo yote, jueni ya kuwa yu karibu, milangoni."_
*Utangulizi*
Yesu hakutuambia tarehe ya kurudi Kwake *Mathayo 24:36*. Lakini alitupa alama k**a taa za barabarani — zikitaka tusinzie, tubaki macho na tayari *Mathayo 24:42*. Hizi ni _mwanzo wa utungu_ *Mathayo 24:8*, si mwisho wenyewe.
---
*1. Vita na uvumi wa vita - Mathayo 24:6-7*
*Biblia yasema*: _"Mtasikia habari za vita... taifa litaondoka juu ya taifa."_
*Mfano leo*: Vita Ukraine-Russia, Gaza-Israel, DRC mashariki, Sudan. Mataifa yanaongeza silaha. Uvumi mtandaoni unatisha kila siku.
*Funzo*: Usishtuke. Haya yapasa kutukia, lakini mwisho bado *Mst. 6*.
*2. Njaa, Tauni na Matetemeko - Mathayo 24:7*
*Biblia yasema*: _"Kutakuwa na njaa, na tauni, na matetemeko ya nchi."_
*Mfano leo*:
- *Njaa*: Milioni 700+ wana njaa 2026 — Yemen, Pembe ya Afrika, Gaza.
- *Tauni*: COVID-19, sasa Mpox, Ebola, Kipindupindu.
- *Matetemeko*: Uturuki 2023 watu 50k+, Morocco, Japan.
*Funzo*: Dunia inatetemeka. Lakini Mungu ni mwamba wetu *Zaburi 46:1-3*.
*3. Ongezeko la Uovu - 2 Timotheo 3:1-5, Mathayo 24:12*
*Biblia yasema*: _"Watu watakuwa wakijipenda wenyewe... upendo wa wengi utapoa."_
*Mfano leo*: Utapeli mtandaoni, biashara ya binadamu, watoto kutotii wazazi, watu kujali “mimi kwanza”.
*Funzo*: Usiruhusu moyo wako ubaridi. Endelea kupenda hata uovu ukizidi.
*4. Injili Kuhubiriwa Ulimwenguni Kote - Mathayo 24:14*
*Biblia yasema*: _"Injili hii ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote... ndipo ule mwisho utakapokuja."_
*Mfano leo*: Biblia kwa lugha 3600+. Injili kwenye YouTube, TikTok, WhatsApp. Wamisionari hata Korea Kaskazini.
*Funzo*: Kazi haijaisha. Kila mmoja wetu ana sehemu ya kuhubiri.
*5. Manabii wa Uongo na Mafundisho Mapotovu - Mathayo 24:11, 24*
*Biblia yasema*: _"Manabii wengi wa uongo watatokea... hata wateule wangeweza kudanganyika."_
*Mfano leo*: “Panda m