Kanisa la Yesu kristo R d congo

Kanisa la Yesu kristo R d congo Matumaini ya mwamini yako katika Yesu Kristo mwenye nguvu zote ajuaye yote aliyeko wakati wote .

KITABU HIKI KIPO DISPONIBLE KWENYE LUGHA YA KISWAHILI
06/08/2024

KITABU HIKI KIPO DISPONIBLE KWENYE LUGHA YA KISWAHILI

06/08/2024

BONNE NUIT

17/04/2022

USIANGALIE UKUBWA WA UKUTA ULIOPO MBELE YAKO.

Usiuangalie ukubwa wa ukuta uliopo mbele yako, bali utazame ukuu wa Mungu, naye Mungu atakushindia.

Usiuangalie ukubwa wa mapito unayoyapitia, bali utazame ukuu wa Mungu, naye Mungu atakushindia.

Mungu ni mwenye uweza, hakuna jambo lililogumu mbele zake, yeye anaweza kila jambo. Inawezekana ukawa unapitia magumu mengi yanayokuzuia kufikia mafanikio, yanayokukosesha amani maishani mwako. Inawezekana ni maginjwa, matatizo ya ndoa, na mengine mengi. Wewe mtazame Mungu naye atakushindia.

Hehu tujifunze kwa wana wa Israeli, walipofika Yeriko, walizuiliwa na ukuta mkubwa kuingia ndani ya mji ili kuendelea na safari yao ya kuelekea Kanaani. Ukuta unakuzuia wewe ni hayo mapito unayoyapitia.

Usikate tamaa, Mungu anakuambia hivi k**a alivyosema na Yoshua, "BWANA akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake." (Yoshua 6:2)

Kwahiyo nawe magumu hayo yamekwisha wekwa chini yako kuyamaliza, lililobaki ni wewe kufuata maelekezo ambayo Mungu anakupa ili kuyashinda hayo matatizo.

Wana wa Israeli walipewa jukumu la kuuzunguka mji ule kwa siku sita wakipiga tarumbeta na kelele mbele ya sanduku la agano. Na siku ya saba waliambiwa wauzunguke ule mji mara saba, makuhani saba wakipuliza tarumbeta wakiwa mbele ya sanduku la agano na wengine nyuma wakipiga kelele, na walipomaliza mizunguko yote ule ukuta ulianguka na wakauteketeza ule mji, waliopona ni familia ya Rahabu yule kahaba. (Yoshua 6)

Kwahiyo na wewe usilalamike, bali mwamini Mungu, mtii Mungu, mtegemee Mungu nawe utafanikiwa. Wala usione ugumu wa mambo ambayo Mungu atataka uyafanye ili kuyafikia mafanikio yako au ufumbuzi wa mapito yako.

Ndiyo maana Mungu aliwaambia wale watu wauzunguke mji, unafikiri Mungu asingeamua aungushe tu ule ukuta hata bila kuwaagiza kuuzunguka? Unafikiri angeshindwa? La! Hasha! Asingeshindwa. Bali alitaka aone imani yao kwake na utiifu wao kwake.

Unafukiri wale watu wangebaki kulalamika nje ya ukuta wangefanikisha kupita Yeriko, hapana, wasingeweza.

Ili uyashinde hayo mapito yako, ni lazima uchukue hatua.
(a) Mwamini Mungu kuwa anaweza hata yale yasiyowezekana (Yeremia 32:27, Luka 18:27)
(b) Ishi maisha matakatifu.(1Petro 3:13)
(c) Soma, jifunze, tafakari Neno la Mungu kila wakati, kwani huko ndiko kuna majibu ya mahitaji yako yote (Yoshua 1:8)
(c) Kila unalolifanya, lifanye kwa jina la Yesu, (Wakolosai 3:17)
(d) Omba bila kukoma,(1Wathesalonike 5:17)

Usimuogope adui yako, bali kabiliana naye kwa kumtegemea Mungu katika jina la Yesu Kristo aliye hai, maana yeye ni mshindi tangu enzi na enzi na hata milele, nawe utashinda.

Na ukisha shinda, watu wote watamtukuza Mungu aliye hai juu mbinguni na habari zake zitaenea kwa watu wote.
"Basi BWANA alikuwa pamoja na Yoshua; sifa zake zikaenea katika nchi ile yote." (Yoshua 6:27)

Kwahiyo mpendwa usiuangalie ukubwa wa ukuta(matatizo/mapito) uliopo mbele yako, bali utazame ukuu wa Mungu, naye Mungu atakushindia.

Mungu akubariki sana.

10/04/2022
06/04/2022

Baba Mtakatifu, Mungu Mkuu sana, Mweza wa mambo yote, ninakushuru kwa ajili ya wema na fadhili zako ambazo zimekuwa pamoja nasi usiku wote na hatimaye umetuamsha salama. Asante kwa mambo yote ambayo umetutendea usiku mzima ikiwemo kutulinda na kutuepusha na mabaya yote ambayo shetani alitukusudia. Pokea sifa na heshima na utukufu kwa wingi wa wema na fadhili zako Ee BWANA.

Naomba kwa huruma na rehema zako utusamehe dhambi na uovu na makosa tuliyokutenda siku ya leo. Tusamehe sisi na watoto wetu na wazazi wetu na wenza wetu na kanisa lako na taifa letu la Tanzania. "BWANA k**a wewe ungehesabu maovu yetu Ee BWANA, nani angesimama? Ninakushuru kwakuwa kwako kuna msamaha ili Wewe uogopwe" 130: 3-4.

Baba tembea na watu wako katika shughuli mbali mbali za siku ya leo na kuwajalia kufanikiwa wote wanaokutegemea Wewe. Wamekumbilia Wewe Bwana ili wasiaibike katika kazi zao, katika uchumi wao na biashara zao, katika mashamba yao na katika mifugo yao. Hakuna aliyekumbilia Wewe akiwa analia akarudi ameweka mikono kichwani kwa huzuni bali kila aliyekujia kwa machozi alirudi akishangilia. Ingilia katu na uwafundishe watu wako kufanya mambo yote ili wapate faida maana Wewe ni Mungu Mkombozi wetu utufundishaye ili tupate faida 48:17.

Mungu wetu uliyetuumba, naomba sana uondoe magonjwa yote ya kufisha na kutaabisha katika taifa hili la Tanzania na nchi nyingine nyingi za Afrika na Dunia nzima. Ondoa vita na machafuko yanayoendelea kwenye mataifa mbalimbali hasa mataifa ya Ukraine na Russia maana Wewe U Mungu wa amani si wa machafuko 14:33.

Siku ya leo nakuomba Mungu wetu ukawe Mwalimu Mwema kwetu ili utufundishe yatupasayo kwenye maeneo yote ya maisha yetu kwakuwa Wewe BWANA Mungu ni Mungu Mkombozi wetu utufundishaye ili tupate faida na utuongozaye katika njia itupasayo kuiendea 48:17.

Tuongezee imani Ee BWANA tunapoifanya kazi yako Mungu wetu. Maana imani ndiyo ngao ya kuizima mishale yote yenye moto ya mvovu ibilisi shetani. Mishale ya magonjwa,taabu, njaa na masumbufu ya dunia hii hatutaweza kuizima pasipo imani. Tupe neema ya kuvaa kisawasawa ngao ya imani 6:16.

Baba, naomba neema ya ulinzi wako iwe pamoja nasi siku hii ya leo ukatuepushe na kila hila mbaya za adui. Tulinde na kutuepusha dhidi ya wachawi, ajali katika safari zetu zote, pepo wa chafu, mauti, magonjwa na nguvu zote za giza ili tupate neema ya kushinda salama na kulitumikia kusudi lako.

Baba, utukuzwe milele. Ni katika jina la Yesu Kristo nimeomba na kushukuru. Amina!

"YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU YAWEZEKANA KWA MUNGU" 18:27.

Ikiwa unabarikiwa na huduma zetu wasiliana nasi kwa namba zifuatazo ili tukuhudumie;

O758443873 au
+255763798746.

Mpendwa mwana wa Mungu nakukaribisha uungane nasi katika maombi ya kufunga na kiomba kwa masaa 12 kuanzia saa 12 asbh mpaka saa 12 jioni kila siku ya Ijumaa-Jumapili tukiombea kanisa, taifa na kujiombea wenyewe pamoja na familia zetu.

Nakutakia J3 njema yenye baraka tele.

04/03/2022

Adresse

Masisi
Goma
KANISALAKINIGIMTAANIMASISI

Téléphone

+243898173428

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Kanisa la Yesu kristo R d congo publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Partager