12/12/2025
Somo:Sema Naye(Yesu) anasikia
A. Luka 5:12-13
[12]Ikawa, alipokuwa katika mmojawapo wa miji ile, tazama, palikuwa na mtu amejaa ukoma; naye alipomwona Yesu alianguka kifudifudi, akamwomba akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.
[13]Naye akaunyosha mkono wake, akamgusa akisema, Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukamwondoka.
B. Jinyenyekeze (alianguka) kwa Yesu kristo
C. (i) Yesu kristo ananyoosha mkono (ii) Anagusa mtu (iii) Huponya
Ushauri
Wapendwa tumeona Yesu kristo anasubiri useme shida Yako. Yesu kristo husikia na kujibu au kutekeleza kwa kuondoa shida Yako
Sala
Asante sana Yesu kristo kwa kutuonyesha unasubiri tulete shida zetu kwako. Yesu kristo tunakuja kwako kwa kukuheshimu, kukuabudu na kukusifu kwani baraka na nguvu ziko kwako. Tunaomba utuondolee vikwako ktk maisha yetu, huduma zetu na nchini kwetu ktk jina lako Yesu kristo. Amina
Mwanafunzi wa Yesu. Bishop Moses Amissi Bukavu Drcongo tel 0992112596