19/02/2022
KUJIANDAA KWA AJILI YA MAISHA YA MILELE - 1
Bwana Yesu asifiwe sana!
Wanadamu hawawezi kuepukana na wajibu kwa ajili ya matendo yao.
" Na k**a vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;"(Waebrania 9:27)
Watu wengi hawapendi kufikiria kuhusu kifo na mwisho wa maisha yao hapa duniani. Wanapenda kusikia tu habari za habari za uzima wa milele, lakini hawapendi kusikia habari za jehanamu. Wengine wanathubutu hata kusema kwamba Mungu ni upendo, na kwamba Mungu mwenye upendo namna hiyo hawezi kumpeleka mtu yeyote motoni.
Yatupasa kukumbuka kuwa ya kwamba Mungu HAMPELEKI MTU YEYOTE MOTONI, lakini pia, Mungu huyo huyo HAMZUII MTU ANAYETAKA KUINGIA MOTONI KWA UCHAGUZI WAKE MWENYEWE.
Mungu alimtoa mwanawe, Yesu Kristo, kufa kwa ajili ya wanadamu wote juu ya msalaba, ili watu wote wapate kuwa na njia ya wokovu. Upendo wa Mungu unaonekana katika kifo cha Mwana wake mpendwa, Yesu Kristo.
Kwakuwa mwanadamu ana uhuru wa kuchagua, anaweza kuchagua kuupokea upendo wa Mungu na mafanikio yote yanayofuatana na tendo hilo, au anaweza kuchagua kukaa katika dhambi na baadae kuteseka kwa ajili ya dhambi hiyo.
Biblia inaeleza wazi wazi ya kwamba kuna mahali namna mbili, MBINGUNI ambako ni pa baraka na furaha. Na MOTONI ambapo na mahali pa huzuni na kusaga meno.
Tunawezaje kuacha kujali wakati ujao na kujitayarisha kwa ajili ya umilele, wakati ambapo Yesu mwenyewe katika somo hili anasema wazi kuwa kuna moto?(Luka 16:23-25)
K**a tutahitaji kuelewa zile habari ambazo zinatajwa katika somo hili kwa vizuri zaidi, ni lazima kwanza tufahamu mambo yale tunayofundishwa na Agano la kale kuhusu maisha ya wakati ujao. Neno ambalo limetumiwa kuwa ni moto, ni tafsiri ya neno la Kiyunani ambalo ni "Jehanum" na hilo linatumiwa katika Agano Jipya lililoandikwa katika lugha ya Kiyunani, nalo ni sawa na neno la Kiebrania ambalo ni "Sheolo" lililotumiwa katika Agano la Kale la Kiebrania. Kulikuwa na sehemu mbili, sehemu ya kwanza ilikuwa inahusika na mateso kwa watu waovu, na sehemu ya pili ilihusika na mahali pa faraja kwa ajili ya watu wema.
Mahali hapo pawili hapakuwa na mwisho kwa ajili ya mapumziko ya ambao ni waovu au watu wema.
Wakati Yesu alipokufa aliwachukua watu wote wema mbinguni, na sasa wale wanaokufa katika Kristo wanakwenda moja kwa moja kuwa na Bwana, maana wameokolewa kutoka katika dhambi zao, Biblia inasema, "Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao." (Ufunuo 14:13)
Watu wale ambao hawajaokolewa wanakwenda motoni ambako wanangojea kwa mateso makali, hukumu ya mwisho ambapo jehanum itageuzwa kuwa bahari ya moto iwakayo milele na milele, (Ufunuo 20:14; 21:8)
Litaendelea......
Mungu akubariki sana.
đź–Š Mwl. Lazaro Zakaria
Instagram: http://www.instagram.com/lazarozakaria_
Telegram: http://t.me/SomaNenolaMungu
http://t.me/NenolaMungu
Mungu akubariki sana!